Wanaume tuweni serious tusicheze na hisia za wachumba zetu, nashangaa kuona mtu anatoa mpaka posa anapangiwa mahali halafu anamkimbia binti hamuoi anaenda kuoa mwanamke mwingine, sijui tatizo huwa ni nini.
Hilo suala nishawahi kulishuhudia zaidi ya mara mbili.
Lengo la kwanza huwa ni kukomoa na kudhalilisha, lengo la pili ni uhuni.
Nitaeleza visa hivi kifupi sana.
Kisa cha kwanza ni kama kukomoa: kuna msichana aliyejitunza vyema na akawa ni mfano kijijini kwao.
Kila kijana aliyemtaka kimapenzi alikataliwa na msimamo wa msichana ikawa kijana atakayemsikiliza ni yule mwenye malengo ya kuoa tu.
Mhuni mmoja akaigiza kumchumbia, taratibu za washenga na posa akatoa, ila kutangaza ndoa akawa anatoa visingizio kuvuta muda.
Kwa kuwa ameaminiwa na mchumba pamoja na wazazi, akawa anamchukua mchumba wake huyo mbele ya wazazi bila ya wasi wasi kwenda naye mjini kumnunulia vitu na huko msichana akalaghaiwa, jamaa akawa "anajisevia".
Na mwisho wa siku jamaa kaingia mitini huku lengo lake kalitimiza kauli mbiu yake ikiwa ni: ..."kwani pesa kitu gani kupoteza?"
Kisa cha pili mtiririko wa kuanzia unafanana na kisa cha kwanza, kuchumbia na kisha kufanya mapenzi kabla ya ndoa.
Sasa huyu alikuwa ni kivuruge hasa, ilikuwa afunge ndoa kanisani.
Aliiwatia hasara mpaka wazazi wake kwa kuandaa sherehe ya gharama kubwa na kisha akaingia mitini dakika za majeruhi, bibi harusi na wapambe kutelekezwa na shela lake kanisani bwana harusi asijitokeze na ikaishia hivyo.
Nilichojifunza kwa matukio haya mawili ni kwamba wasichana wenyewe kushindwa kusimamia misimamo yao mpaka mwisho.
Kuwaamini wachumba wao kupita kiasi, hasa mvulana akishamchumbia na kutoa mahari, huaminiwa sana kuwa hatua hiyo huwa si rahisi kubadili mawazo.
Nikija kwa upande wa wazazi: ni kusimamia kwa ufasaha maadili ya dini, mila, desturi na tamaduni juu ya malez bora ya mtoto wa kike.
Mtoto wa kike iwe ni mwiko "kusogeleana" na mchumba wake wa kiume mpaka siku watapofunga ndoa, ieleweke wazi kuwa thamani ya mwanamke hubakia ilivyo asipoguswa tu.
Na pressure ya muoaji ya "kubeba mzigo" hupanda akinyimwa na kuishia kula kwa macho, lakini akipewa ile muhu ya kuchakarika hushuka na mwisho wa siku ndiyo kuaibishana.
Watu hawajali thamani ya pesa zao za mahari na gharama zingine wanazozipata katika prosses hiyo.
Msilaghaiwe na utoaji wa mahari mkaanza kumruhusu mtoto wenu kutoka na mchumbake kabla ya ndoa, mambo yakibadilika aibu ni juu yenu wazazi.