KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Huyu mwanamama atauza kila kitu, ikiwezekana hata baadhi ya makabwela watauzwa kwa wenye nazo.Rais anaenda kukaa USA zaidi ya wiki mbili.
Huko anaenda kufanya shughuli za kiserekali na kubwa zaidi ni Uzinduzi wa filamu ya royal tour.
Kila siku tunaambiwa hii filamu ilitengenezwa kwa pesa kiasi cha bil 7 na sio pesa za Serikali.
Sisi akina Kabwela tukajua ni pesa za akina Greenberg na kampuni yao yao CBS.
Baadae mkuu wa nchi anaibuka akiwa jijini Arusha na kudi kuwa ni pesa zilizochangwa na watanzania.
Je, ni akina nao waliochanga kimya kimya ili kufanikisha Royal tour?
Je, wamejitolea bila hata kutegemea chochote?
Kwa nini zisitumike pesa za Umma? Au ndio kuandaa mazingira?
Kinachosikitisha ni kwamba hakuchaguliwa na yeyote, na wala sera zake hizi hakuzinadi kwa yeyote ili wananchi wamchague ili ayekeleze aliyoahidi.
Yeye kadandia tu kwa Mwendazake, kimya kimya huku akiumia moyoni na mienendo ya basi wake na sera zake, kumbe alikuwa hazikubali kabisa!
Mara vuuu, pera likamdondokea kichwani. Katupilia mbali tena kwa spidi ya radi, yale yote aliyokuwa akiyasimamia bosi, na kuingiza ya kwake bila ya idhini ya mtu yeyote. Si chama chake, wala wanachi.
Hali hii ni udhaifu mkubwa sana katika muundo wa utawala wa nchi yetu.
Mtu kama kaachiwa/karithi serikali, asiruhusiwe kuingiza ya kwake nje kabisa ya yale wananchi waliyokusudia serikali ikayatimize. Kama anataka kuingiza ya kwake, basi aende kwa wananchi wampe baraka zao, lakini siyo kuvamia kwa ujambazi kiasi hiki.