INAKUWAJE: Umekuwa Mbunge, umesoma nje ya nchi, umefanya kazi Obama foundation lakini bado unavizia teuzi za uDC, uRAS ?

INAKUWAJE: Umekuwa Mbunge, umesoma nje ya nchi, umefanya kazi Obama foundation lakini bado unavizia teuzi za uDC, uRAS ?

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
19,629
Reaction score
34,199
Kiukweli serikali iheshimu sekta binafsi.

Kujiajiri kwa mafanikio ni kipaji cha kipekee sana.

Hivi inawezekana vipi Joshua Nassari kutumia pesa za ubunge kwenda kusoma nje, lakini unarudi kutafuta teuzi ???

Lijualikali alikuwa anatafuta teuzi mpaka analia licha ya kuwa na mshahara, posho na mafao ya ubunge.

Kwa hali ilivyo niwapongeze sana GRADUATES mliotoka vyuoni hamna hata 100 isipokuwa deni la bodi ya mikopo halafu mnaambiwa mjiajiri, mnaishi vipi 🤣

Anayetakiwa kujiajiri ni nani kwani na anatakiwa kuwa na sifa zipi ?

Maana tunaodhani wana resources zote za kujiajiri ndio hao wanavizia teuzi tena za uDC!!!!!!
 
Kiukweli serikali iheshimu sekta binafsi.

Kujiajiri kwa mafanikio ni kipaji cha kipekee sana.

Hivi inawezekana vipi Joshua Nassari kutumia pesa za ubunge kwenda kusoma nje, lakini unarudi kutafuta teuzi ???
Wewe kijana roho mbaya inakusumbua sana, siku ukipona ugonjwa wa roho mbaya milango ya kufanikiwa itafunguka kwenye maisha yako.
 
Kiukweli serikali iheshimu sekta binafsi.

Kujiajiri kwa mafanikio ni kipaji cha kipekee sana.

Hivi inawezekana vipi Joshua Nassari kutumia pesa za ubunge kwenda kusoma nje, lakini unarudi kutafuta teuzi ???
Joshua Nassary alipata Ubunge wa CDM akiwa very immature. UDC utakuwa ndiyo mwisho wa career yake kwa kuwa mazingira atakayokutana nayo huko hayatampeleka popote.
 
Hupendi kuona mtu amepata hupendi kuona mtu amesonga mbele. Unaumia sana.
Nani anasonga mbele ?

Hivi unawajua kina MO, marehemu Mfuruki ?

Hawa ni watu waliosoma nje pia.

Mtu aliyekuwa mbunge, aliyeenda kutafuta elimu mpaka ng'ambo akirudi kuanza kulialia kusaka teuzi wewe unaona kapiga hatua kweli ?
 
Back
Top Bottom