Elections 2015 Inang'ara CCM, Kimenuka kwa Wapinzani

Elections 2015 Inang'ara CCM, Kimenuka kwa Wapinzani

Ccm ni Chama bora Tanzania nimelithitisha hili juzi baada ya kusikiliza vizuri hotuba ya Slaa na kumtathimin El na Ufisadi wa Tanzania... nimegundua Magufuli ndio Chaguo sahihi kwetu
 
Pesa imeondoa uadilifu ndani ya vyama vya upinzani kiasi watu makini wenye hoja mathubuti hawapo ndani ya chama, na ndio maana chama hakina ilani wala sera, unapaswa kujiuliza kwa muda lowasa anaingia ukawa na kupewa nafasi ya kugombania ameshiriki kuandika ilani lini hapo ndipo unapopata wakati mgumu kufahamu juu ya maigizo haya yanayoendelea na ndio maana Watanzania wamechoshwa na udanganyifu huu. ccm endeleeni kung'ara mpaka ikulu baada ya ushindi wa 90%
 
Hii chama muzuri sana,miradi ya ujenzi ya bil 500 inagharamiwa kwa sh bil 1400!
 
Bora uandike kidogo lakini ujumbe ufike, lakini siyo kuandika habari isiyo na hoja wala mashiko, nadhani umeelewa. Wapinzani mkiona sehemu imeandikwa CCM mnatetemeka, mkimuona Jakaya mnatetemeka, mkimuona Kinana mnatetemeka, mkimuona Nape mnatetemeka, mkimuona Magufuli mnaumia karibu kuzimia, na mkiona kijani na njano mnateseka sana, habari ndio hiyo

Hahahah ile ya kuongea dakika nane ilinifurahisha, eti mtu anataka urais yupo serious ameongea dakika nane halafu anawaambia watu waende website, these people are not serious, upepo umewabadilikia hivi sasa, watu walijuta kwanini walienda kumsikiliza mtu, wao wametoka mbali halafu anaongea dakika 8 na kuwaambia waende website, hata mgombea ujumbe wa shina hawezi kujinadi kwa namna hiyo
 
ccm, mbele kwa mbele, tunataka mafanikio , na maendeleo bora sio bora maendeleo, mjipange wapinzani mwaka mwingine mje na trekta , sio kisu tena butu #hapakazitu

Ukweli mnaujua sana isipokuwa mnajifanya makauzu huu mwaka hamuponi na hilo hata mtoto wa chekechea analijua.bye bye mkoloni mweusi.
 
Hangova ya viroba ikiisha rudia tena kusoma u.pu.pu uliopakaza humu
Na ukimaliza kusoma uende ukamsimulie El na Ukiwa halafu utanunuliwa Viroba vingine ila ccm huku ni juice tu viroba marufuku,mwisho wa viroba kwenye mikutano ya El na Ukiwa:A S-frusty:
 
Ni kweli kabisa ccm ni chama chenye sera mzuri... Kama kuuzwa kwa twiga wetu, madawa ya kulevya kupita Airport bila Tatizo, kivuko cha mwaka 1978 kimenunuliwa Bilion 8, ukienda hospitali wakina mama wanajifungulia chini, Elimu pia ni mzuri kuna mpaka dv 5, kwa kweli ni chama chenye sera mzuri kabisa


Kuna sehemu nimesoma nikabaki nashangaa. Eti wanasema Lowassa ndiye aliyeleta Division 5.
Najiuliza kama Lowassa alishawahi kuwa Waziri wa Elimu sipati jibu bado.
Wacha niendelee kujiuliza. Nikipata jibu ntarudi
 
viroba vilikuwepo jangwani 29th, mpaka babu yenu akalewa harufu tu maskini. lowasa anaita luwasaa bwahahahha CCM mbele kwa mbeleeeee

hahhaha, nasikia hadi harufu ya mmea ilisikia siku hiyo. cant blame them. ni sera za hiyo chama cha ukasikazini inatifua akili zao 1661150_116610198692034_6074403709178558733_n.jpg
 
Hayo ni maneno yako badilika@ ww Ccm sio baba hako lowassa mbele kwa mbele

Baba yake siyo ccm, lakini pia na wewe Lowasa siyo baba yako, Lowasa ni ccm B, kwahiyo wewe kama unampenda Lowasa basi kaa ukijua unaipenda ccm, kama walivyotengua kauli zao mf, MBOWE: "Lowasa chadema over my dead body" SLAA: ";Lowasa fisadi" watabadilika tu, warudi CCM walikotoka, na CCM watamkuta mzee Magufuli na mahakama yake ya mafisadi, sijui nini kitatokea hapo
11986326_800511963394832_4135627280586118916_n.jpg
 
Nje ya serikali ila NI mwanachama Na mjumbe Wa kamati kuu NEC pia mjumbe meza kuu CCM ambayo ndio Chama chenye Dola mpaka sasa. So Ilani ya sasa anaijua in and out. Na mipango yote anajua. Kumbuka mambo yaki shindikanaga Bungeni wanaitana kwenye kikao cha Chama haraka baada ya vikao Vya Bunge. Una semaje yuko Nje. Wakati pia NI mzee mshauri Wa Chama toka 2009.

Kwahiyo unasema ni kheri hayo maharamia 200 kuliko huyu mmoja lowassa?Bora nichague huyu mmoja aliyejiunga na watanzania kuliko kundi lile lenye malengo yaleyale
 
UKAWA TOLEO JIPYA HAIFAI KUPEWA DHAMANA YA KUONGOZA TAIFA HILI PENDWA LA JMT, NI GENGE LA WAHUNI, WASALITI WA MISINGI YAO, VIGEUGEU, WANAFIKI NA WAZANDIKI WALIOTUKUKA, watanzania hatupo tayari kuuza nchi yetu, TUMESHASEMA KWA WINGI KUWA HATUTACHAGUA UKAWA TOLEO JIPYA.
Mliotolewa ufahamu endeleeni na UZEZETA WENU.

Kula like angu
 
Baba yake siyo ccm, lakini pia na wewe Lowasa siyo baba yako, Lowasa ni ccm B, kwahiyo wewe kama unampenda Lowasa basi kaa ukijua unaipenda ccm, kama walivyotengua kauli zao mf, MBOWE: "Lowasa chadema over my dead body" SLAA: ";Lowasa fisadi" watabadilika tu, warudi CCM walikotoka, na CCM watamkuta mzee Magufuli na mahakama yake ya mafisadi, sijui nini kitatokea hapo
View attachment 283254

Kwahiyo na Slaa alikuwa ccm b?Hiyo mahakama ya mafisadi unadhani atawapeleka Mkapa na Jk?Watapelekwa malofa kutolewa kafara tu,hiyo ni danganya Toto!
Tumeamua kuchagua cdm,viva Ukawa!
 
nina hakika umeandika na kupost haraka lakini ukasahau kuwa hapo ulipo zahanati iko mbali na una tabu ya maji kwa miaka 54
 
Watanzania sasa hasa wafuasi wa ccm hawajadili hoja,wanakalia kujadili mambo ya kijinga kijinga badala ya kuhoji vitu vya msingi,taifa linamalizwa na tunabebeshwa madeni makubwa kwa uzembe wa serikali,badala ya kuwahoji hayo kwenye mikutano ya kampeni tumekalia vijembe!
Magufuli aulizwe kwanini wizara yake ilipe bil 1400 kama faini badala ya billion 500 ambayo ndio gharama halisi ya miradi?Kwanini huo mzigo tubebeshwe wananchi?
 
Kwahiyo unasema ni kheri hayo maharamia 200 kuliko huyu mmoja lowassa?Bora nichague huyu mmoja aliyejiunga na watanzania kuliko kundi lile lenye malengo yaleyale

Tunataka mabadiliko kupitia CCM, mauzauza ya vyama pinzani tumeyachoka, hawaeleweki, kwanza wanatengua kauli zao wenyewe halafu pili, wanagongana kauli wenyewe, tumuelewe nani na tumuamini nani. Hapa CCM tu na Magufuli
 
Yani safari hii jiwe moja wote puuuuuhhh....afu wasipo angalia Zitto na ACT wana rudi na wabunge wengi

Hahahah, siyo jiwe, maana walisema mtu mzima akizidiwa anakimbilia jiwe, tunawapuliza tu kwa upepo, mawe tutawaua
 
Back
Top Bottom