Inaposemwa mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja huashiria kwamba hata mkeo anaweza kuwa wa mwanaume mwingine

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
6,514
Reaction score
15,247
Imezoeleka kusemwa kwamba mwanaume katu hawezi kuwa wa mwanamke mmoja ila lazima awe na wanawake wengi,je umeshawahi kujiuliza kwamba huyo mwanaume ambaye hakai na mwanamke mmoja kwamba anaweza pita na mkeo?

Kama hivyo ndivyo basi nadhani wanaume ifike kipindi tujue kwamba kama sisi hatuwezi kukaa na mwanamke mmoja,na tunawaendea wanawake wa wenzetu basi hata wanawake wetu nao watafuatwa na wanaume wenzetu,yani iko hivyo.

Kwa maana nyingine tutaendelea kubadilishana kwa stahili hiyo,sasa tuache kujifanya tuna wivu sana wa kupindukia mipaka mpaka kuchinjana na kutoana vilema wakati sote ni wakosefu

Huyo mwamba wa Guinea Bartasar ametuonyesha kwamba hakika wake zetu wanaliwa sana ni hivyo hatujui tu,na kutojua kwetu ndio uzima wetu,tunaweza lea familia na kufanya majukumu mengine kama kawaida,vinginevyo tungekuwa na msongo wa mawazo na ufanisi wetu kupungua.

Kwahiyo usaliti ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kasoro wale ambao hakika wamebarikiwa kwa kuwa na hofu ya Mungu,binafsi naamini kabisa hakuna kinacho muongoza mwanadamu katika njia ilinyooka isipokuwa ucha mungu wa kweli,lakini nje ya hapo,ni ngumu sana kwa mwanadamu kukwepa vishawishi na tamaa.

Na tumeona hao wake za watu ambao wamepitiwa na huyo legend wa Guinea hawana dhiki ya maisha,wana maisha mazuri sana kwakuwa wengi ni wake za watu mashuhuri,ina maana kwamba usaliti ni zaidi ya pesa na maisha mazuri,ni tamaa ya asili ya mwanadamu

Kwahiyo wanaume tunapo endeleza ile kasumba ya kusema mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja,basi tambua hata mkeo atakuwa windo la mwanaume ambaye hakai na mwanamke mmoja,sijui nimeeleweka?

Mwisho tusiogope kuoa na kuolewa kwa haya yanayotokea,kwani ndoa ni takwa la muumba wetu,hivyo ni wajibu kama wanadamu kutekeleza hilo ili tuzae na kuendeleza familia bora

Inasemwa bora ni kuwa na huyo mmeo au mkeo ambaye amekuchagua wewe kati ya wengi kuwa mshirika wako wa maisha,hilo ndio jambo kubwa hayo mengine ni matokeo kwani moyo wa mtu ni kichaka.

Furahia ndoa yako kwa moyo mmoja mpaka pale yatakapo kuja kudhihirika usiyo yatarajia,ila usitayafute majanga ila wewe yawache mpaka yatakapo jidhihirisha yenyewe.

Ndoa bado itabakia kuwa hitajio muhimu sana kwa mwanadamu,ilikuwa hivyo na itaendelea kuwa hivyo dahari na dahari pamoja na changamoto zake

Ni hayo tu!
 
Mwanamke hawezi kuwekeza hisia sehemu mbili au zaidi kwa wakati mmoja ila mwanaume anaweza na hapawezi kua na shida.
Kweli kabisa boss,ndio huyo mwamba pamoja na kula wanawake 400+ bado mkewe hakujua chochote,wanaume tunaweza kutenganisha kati ya mke na hawara,,lkn mwanamke anawekeza hisia zote kwa mchempuko mpya,ingawa ni wachache sana wapo smart
 
Kwahiyo sahivi uko wapi?
 
Zinaa ni kama deni tu, ukigonga mke wa mtu na wewe mkeo atagongwa, ukigonga mtoto wa mtu na wewe mtoto wako atagongwa, ukigonga dada wa mtu na wewe dada yako atagongwa, ukigonga mama wa mtu na wewe mama yako atagongwa.
Kiufupi kuna watu hua hawazini bali wanalipa tu madeni ya watu wao wa karibu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kweli kabisa boss,ndio huyo mwamba pamoja na kula wanawake 400+ bado mkewe hakujua chochote,wanaume tunaweza kutenganisha kati ya mke na hawara,,lkn mwanamke anawekeza hisia zote kwa mchempuko mpya,ingawa ni wachache sana wapo smart
Kwani hao wanawake walio liwa na huyo jamaa waume zao walikuwa wanajua sio?
Mungu amesha haramisha uzinzi kwa watu wote iwe mwanaume au mwanamke , uzinzi ni uovu kama uovu mwingine.
 
Hiyo wengi walichelewa kujua.

Mwanamke pia anaweza kuolewa na Wanaume wanne Kwa pàmoja kama ilivyo Sisi Wanaume tunavyoweza Kuoa Wake Weng
 
Kwani hao wanawake walio liwa na huyo jamaa waume zao walikuwa wanajua sio?
Mungu amesha haramisha uzinzi kwa watu wote iwe mwanaume au mwanamke , uzinzi ni uovu kama uovu mwingine.
Walikuwa hawajui ndio maana huwa napinga sana kuchungazana kwa wanandoa,kama kuna sintofahamu huwa naamini ipo siku itajulikana

Wengi wetu tunajua zinaa ni njia mbaya ila bila kumuelekea Mungu kwa ibada na kuwa waja wema ni ngumu kutoboa
 
Back
Top Bottom