Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Inaelezwa kuwa baadhi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki hapa nchini wamemvaa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima, na kumtaka kujitokeza kufafanua ni kwanini amekua akiendesha vikao vya siri vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bila kuutarifu uongozi wa kanisa hilo.
Maaskofu hao wamehoji ni nani aliyemtuma Padri Kitima kuitisha mikutano ya kujadili nani awe mgombea uenyekiti wa Chadema Taifa na nani awe mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
"Kiukweli Maaskofu wamechachamaa katika kundi la WhatsApp, na wengine wanaandika SMS za kumuuliza jambo hili ila Padri Kitima amekaa kimya tu bila kujibu. Ameulizwa aliitisha vikao kama Katibu wa Baraza la Maaskofu au kama kada wa CHADEMA?", kimeeleza chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TEC.
Pia, Soma: Kuna vita ya chinichini inaendelea dhidi ya viongozi wa dini wanaokosea Serikali
Itakumbukwa kuwa juzi Tundu Lissu aliwaeleza wanahabari kuwa, ni kweli yeye na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe waliitwa katika kikao cha siri kilicholenga kuwasuluhisha na kujadili jinsi viongozi hao nafasi ya uenyekiti na nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania.
Kupata matukio mengine kuelekea Uchaguzi 2025: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025