Pre GE2025 Inasemekana baadhi ya Maaskofu wachukizwa na Padre Kitima kufanya Vikao vya Siri na CHADEMA

Pre GE2025 Inasemekana baadhi ya Maaskofu wachukizwa na Padre Kitima kufanya Vikao vya Siri na CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe ndio huwezi kuzipata! Kwani hujui kuwa Maaskofu wengine ni ndugu zetu. Pia wengine tumebobea kwenye udukuzi wa mitandao🤣🤣
Labda kama wewe umedukuliwa na wazanzibari na popo bawa
 
Gentleman,
jikite kwenye hoja mahususi mezani kuliko kubabaika na mihemko na makasiriko na kutaja vitu ulivyo navyo mwenyewe,
ama ndiyo ile nyani haoni kundule 🐒
Ni lugha ya picha nadhani shuleni wewe ulienda Kwa sababu ilikua ni kawaida! Huyo ni kalio ambalo huwekwa sehemu yoyote bila idhini yake. Kwani hukusoma ilivyoandikwa? :
Mathayo 5:9
Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Na andiko jingine likasema:
Yakobo 3:16
Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
Huyo afaa kufananishwa na hayawani mana hata Yesu mwenyewe alimwita Herod Mbweha sababu ya upumbavu ulioshinda huu:
Luka 13:32
Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
 
huyo ni mpatanishi au muendekeza udini na kabila?

mpatanishi hawezi kua mnafiki kama huyo katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania, anaeipenyeza chadema ndani ya kanisa katoliki Tanzania.

anawapatanishaje watu waliosema hadharani kwamba hawana tofauti wala uhasama kati yao, kama sio kimbelembele tu?🐒
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Wakuu

Inaelezwa kuwa baadhi ya Maaskofu wa Kanisa Katoliki hapa nchini wamemvaa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima, na kumtaka kujitokeza kufafanua ni kwanini amekua akiendesha vikao vya siri vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bila kuutarifu uongozi wa kanisa hilo.
View attachment 3198009
Maaskofu hao wamehoji ni nani aliyemtuma Padri Kitima kuitisha mikutano ya kujadili nani awe mgombea uenyekiti wa Chadema Taifa na nani awe mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

"Kiukweli Maaskofu wamechachamaa katika kundi la WhatsApp, na wengine wanaandika SMS za kumuuliza jambo hili ila Padri Kitima amekaa kimya tu bila kujibu. Ameulizwa aliitisha vikao kama Katibu wa Baraza la Maaskofu au kama kada wa CHADEMA?", kimeeleza chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya TEC.

Pia, Soma: Kuna vita ya chinichini inaendelea dhidi ya viongozi wa dini wanaokosea Serikali
View attachment 3198011
Itakumbukwa kuwa juzi Tundu Lissu aliwaeleza wanahabari kuwa, ni kweli yeye na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe waliitwa katika kikao cha siri kilicholenga kuwasuluhisha na kujadili jinsi viongozi hao nafasi ya uenyekiti na nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania.

Kupata matukio mengine kuelekea Uchaguzi 2025: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Naye anawakati wa kuwa Kitima kama mpigakura huru na kuna wakati ni askofu ndani ya kanisa, huyu wa KKKT yeye ni CCM namba moja muda wote.
 
Gentleman,
huyo ni mpatanishi au muendekeza udini na kabila?

mpatanishi hawezi kua mnafiki kama huyo katibu mkuu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania, anaeipenyeza chadema ndani ya kanisa katoliki Tanzania.

anawapatanishaje watu waliosema hadharani kwamba hawana tofauti wala uhasama kati yao, kama sio kimbelembele tu?🐒
"muendekeza udini na kabila?" Lissu mkatoliki, Mbowe mluteri. Lissu msingida na Mbowe mkilimanjaro, sasa udini na ukabila uko wapi?
 
Back
Top Bottom