Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,469
- 12,391
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema Nape Moses Nnauye amevuliwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi kufuatia kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti jijini Dar es salaam leo...
Habari hizi ni za kunyapia nyapia zinasema hata Lazaro nae yuko matatani.
Nape Nnauye alikuwa ni waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano kabla uteuzi wake kutenguliwa. Aliteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Pombe Magufuli. Yeye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama lililoko mkoani Lindi.
Hivi sasa Nape ana miaka 40 alizaliwa mkoani Mwanza Novemba 7, 1977 ambako mama yake mzazi alikuwa mfanyakazi katika sekta ya elimu. Mama mzazi wa Nape anaitwa Keziah, ni mwalimu ambaye amefanya utumishi wake hadi alipostaafu mwaka 2015 akiwa katika ngazi ya Ofisa Elimu wa wilaya anayeshughulikia takwimu. Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.
Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara.
Uzoefu mkubwa wa Nape katika masuala ya Uongozi umejikita katika masuala ya siasa zaidi kuliko “utaalamu”. Amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa tangu mwaka 2002 hadi 2012. Amekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa kuanzia mwaka 2002 hadi leo.
Mwaka 2010 hadi 2011 aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Masasi, mahali alikotumikia kwa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mwaka 2011 na kisha mwaka huohuo akateuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa nafasi aliyoishikilia hadi mwishoni mwa mwaka 2015.
Nape alianza harakati za kusaka ubunge mwaka 2010, alishiriki katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ndani ya CCM katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam bila mafanikio (aliyeshinda kura za maoni ni Hawa Ng’umbi aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii wakati huo). Mwaka 2015 Nape alihamishia majeshi nyumbani kwao, jimbo la Mtama. Bahati kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba mwanasiasa nguli ndani ya CCM, Bernard Membe alikuwa ameshatangaza kuliacha jimbo hilo ili agombee urais.
Nape akapambana na kushinda kura ya maoni ndani ya chama chake kwa kupata kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Mathew (mchezaji wa zamani wa Yanga) aliyepata kura 4,766 (baada ya kushindwa Selemani alihamia Chadema na kugombea kwa tiketi ya chama hicho). Kura za jumla zilizopigwa Oktoba 25 zilimtangazia Nape ushindi wa jumla wa kura 28,110, Mathew wa Chadema akatokea wa pili kwa kupata kura 13,918 huku mgombea wa CUF akishikilia nafasi ya tatu.
Nguvu
Mambo mawili makubwa yanajenga nguvu na uwezo wa Nape katika siasa za sasa. Kwanza, huyu ni mmoja wa wanasiasa vijana wenye nguvu na ushawishi mkubwa wa maamuzi ndani ya CCM. Mchango wake kwenye siasa za jumla za kuiimarisha CCM katika miaka ya hivi karibuni hauwezi kupimika. Yeye ndiye mwanasiasa kijana wa CCM aliyefanikiwa kuzunguka sehemu kubwa ya nchi akiinadi CCM kwa kutumia staili ya “kushambulia chama chake” akishirikiana na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana. Staili ile kwa kiasi fulani iliisaidia CCM kujadiliwa tena na wananchi, wengi wakianza kuona kuwa kumbe hata viongozi sasa wanasema hadharani kuwa chama kina matatizo ya maadili na mengine mengi.
Kukaa ndani ya CCM muda mrefu na kusimamia mambo mengi ya mabadiliko ya kimfumo ndani ya chama hicho kunamfanya Nape awe mmoja wa vijana wa sasa ndani ya CCM wanaokifahamu chama hicho kwa undani. Uzoefu wa namna hiyo ni jambo kubwa na umemjengea uwezo wa kutosha na uzoefu wa kujua wapi kuna matatizo gani yanayohitaji ufumbuzi wa aina gani. Hili ni jambo kubwa sana kwake japokuwa tutaendelea kupima utendaji wake.