Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
INASHANGAZA KIJANA ANASIMU KUBWA LAKINI ANASEMA HANA OFFICE WALA KAZI.
Anaandika, Robert Heriel Mtibeli.
Shahidi.
Moja ya mambo yanayonifanya nishangae ni kuona kijana wa miaka 18 -40 mwenye simu kubwa lakini anakuambia sina office, sina kazi, na analalamika, anashutumu, analaani watu wengine.
Nyuma kabisa niliandika mambo mengi sana, na Mungu ndiye Shahidi. Niliandika bure kabisa, kwa nia ya bure kabisa, bila kuhitaji malipo. Nilifanya hivi kwasababu Mimi ni Mtibeli. Na sisi Watibeli tunapenda mafanikio ya watu wote.
Ndio maana nilitumia uelewa, upeo na kile nilichojaliwa kutoa elimu kwa watu, hasa wale wasio bahatika kusoma, wasiobahatika kujua kingereza, wasiokuwa na watu wa karibu wenye kujua mambo haya.
Niliwaambia vijana; ni muhimu kujenga Jina lako. Jina lako ndio litaamua ufike umbilical upi. Lazima ujenge na ulinde Jina lako.
Nilisema, Jina lako litadumu nakupewa heshima kama utasaidia maisha ya wengine kwa kuwapa huduma nzuri.
Na hii ingehitaji uaminifu wako, weledi na umahiri katika kile unachokifanya.
Na hata ukikosea usisite kukubali kukosolewa.
Nilisema Elimu na ujuzi ni muhimu.
Kisha nilisema lazima uwe na Anuani ya Kile unachokifanya.
Na hii ndio mada ya leo. Naam leo nitarudia kufafanua yale niliyowahi kuyaeleza.
OFISI ni eneo lako la kazi. Sio kazi za nyumbani. Kazi kwa maana ya shughuli yoyote inayokuzalishia kipato na kukupa riziki. Hiyo ndio maana ya kazi kwa sisi Watibeli.
Ofisi inaweza kuwa nyumbani kama unafuga kuku, Bata, unatengeneza vitafunwa, na huduma zingine.
Ofisi inaweza kuwa shambani, au machungani, n.k.
Ofisi inaweza kuwa ni udereva, hotelini,shuleni, hospital, magereza, mahakamani,sokoni. N.k.
Kijana wangu, katika maisha yako elewa kuwa Ofisini,sehemu inayokupatia hela ni eneo takatifu, ni eneo kama ulilolitenga kuabudia, kumwita Mungu wako.
Heshimu Ofisi yako. Ni takatifu. Hivyo ndivyo Sisi Watibeli tulivyo.
Usilete mizaha ofisini.
Pafanye pawe Safi.
Hudumia watu kwa uaminifu na heshima.
Sio unaingiza wanawake ofisini. Au unakubali watu wanakuja kufanyia ufuska ofisini kwako.
Mtu anakuja anavuta marinara, au anapachafua ofisini kwako. Hapana. Hiyo sio heshima. Hujiheshimu wewe.
Mtu anatupa tupa hovyo uchafu ofisini kwako unamuangalia kama lijinga hivi.
Unakuta upo kwenye Fremu yako. Mtu anatupa Ganda la pipi au tunda. Wewe unaona kawaida. Mpuuzi wewe. Jiheshimu. Usikubali mtu adharau ibada yako.
Akitukanwa Muhammad na Yesu usiyemjua unapiga kelele nusu kumpiga. Lakini mtu akidharau kazi na eneo la kazi yako unaona kawaida. Chizi wewe.
Unaenda ofisini, unanuka jasho hujaoga, unanuka mdomo hujasafisha meno, unanuka mavi. Alafu unataka upate pesa.
Hapana. Jipende na jiheshimu. Ndivyo Watibeli tulivyo.
Vaa upendeze. Sio lazima uvae nguo za gharama. Vaa ulizonazo. Ulizobarikiwa. Safi zilizonyooshwa.
Kiasi kwamba mtu akikuangalia ukija au ukiwa ofisini anasema naam huyu ndiye kijana/binti anayestahili kunihudumia.
Uso wenye nuru ya furaha,usafi na tabasamu. Sio umenuna kama komodo.
Ofisi sio tuu uwe nayo physically.
Mungu yupo kurahisisha maisha.
Ndio maana aliumba watu watakaorahisisha maisha kwa namna mbalimbali.
Wapo wamele technology ya Mitandao ya kijamii. Hao wote wamefanya hivyo kwa kusudi la Mungu. Maisha rahisi. Yaliyorahisishwa.
Tumia Mitandao ya kijamii kama Ofisi yako. Rahisishia watu wengine maisha.
Kuwa Winga, dalali. Rahisishia wateja na watu kupata bidhaa au huduma fulani. Usiwe lijinga jinga.
Ili ufanikiwe lazima urahisishe maisha ya watu wengine. Uwahudumie.
Nimemaliza kibabe. Lakini sitaki ngumi.
TaikonMaster
Kwa sasa Upanga, Dar es salaam