Hivi mtoa Thread sijamuelewa, kwani tatizo hapo liko wapi? Ni namba ndio zinamchanganya au ni nini?
Najaribu kuichambua hotuba/taarifa ya mama kama ifuatavyo:
- Mwezi wa sita 2021, taarifa ya mama inasema akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 4765
- Mwezi disemba (yaani baada ya miezi sita hivi) akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 6253
Sasa kosa liko wapi kwa sababu akiba imeongezeka toka dola bilioni 4765 mpaka dola bilioni 6253 au ongezeko/tofauti ni dola bilioni 1488. Tupo pamoja jamani! Nisahihisheni nilipokosea.