A
Anonymous
Guest
Juzi kati hapo baadhi ya walimu wanaojitambua halmashauri ya Muleba mkoani Kagera walimwendea mkurugenzi kudai haki yao kuhama CWT kwenda CHAKUHAWATA kwenye makato nafuu (elfu 5 tu haijalishi unapokea ngapi tofauti na CWT wanaokataa 2% ya PAYE yako).
Wakiwa ofisini wakiendeleza mazungumzo na mkurugenzi kuwa madai yao yamepelekwa kwa afisa utumishi kwa barua zaidi ya mara 3 lakini hawajasikilizwa wala kujibiwa , ghafla afisa utumishi Secondari (Gerald Mhile a.K.a NGUVU YA BUKU) akaingia ... Mkurugenzi akamshirikisha kuwa suala hili la walimu kulalamika kutoondolewa CWT likoje?
Afisa elimu akadai hao walimu wanaotaka kuhamia Chakuhawata ni wanaharakati yaani vyama pinzani
"Wanafadhiliwa na CHADEMA na CUF kuendeleza harakati zao" afisa elimu
So mkurugenzi asisumbuke nao kuwasikiliza kwani hakuna chama kinachoweza kujiendesha kwa Elf 5 .
Nikili kusema nimeshangaa na kuchefukwa sana kwa kauli mbovu na mbaya kutoka kwa kiongozi anayetegemewa kutetea walimu wake wapate haki yao, lakini kumbe ni ndiye mdidimizaji wa haki za walimu. Tanzania ofisi nyingi zimekuwa zikijiendesha kisiasa sana, afisa elimu yupo kwa ajili ya kuendeleza siasa za kizamani na kikoloni kwenye karne hii.
Mbona kwenye suala la taaluma tunajitoa kufaulisha na kumuondolea zero
Mbona sisi zaidi ya walimu 1000 ndani ya wilaya tumemuunga mkono kwenye suala lake la NGUVU YA BUKU ambao ni mchango wa kumuchangia mwalimu mwenzetu anapofiwa na mzazi au ndani ya familia yake bila kinyongo .
Walimu mnaojitambua shitukeni uyo mtu yupo kuendeleza agenda zisizo na msingi kwenye mambo ya msingi.
Iweje yeye kumbe ana propaganda za enzi za kikoloni ndani ya taasisi ya kielimu ambayo kimwongozo haitakiwi kujihusisha kisiasa kwa namna yoyote ile .
Mkurugenzi alikuwa tayari kutusikiliza na kuyafanyia kazi madai yetu ingawa naye kwa shingo upande , shida imekuwa kubwa baada ya uyu NGUVU YA BUKU kuingia.
Rai yangu kwa wafanyakazi wanaojitambua tuna aina nyingi za viongozi wa aina hii kwenye taasisi nyingi wakiendeleza u-CCM na huku wakiwadidimiza watumishi wao na kuwafanya vipofu na mazezeta kwa masirahi yao maovu.
Kiongozi wa aina iyo hatakiwi kuwepo ofisini anaonyesha ameshiba so akae pembeni awapishe wanaoweza kusaidia wenye uhitaji.
Jamii Forums na mitandao mingine ya kijamii tunaomba mtupaazie sauti kadri inavyowezekana .