Inasikitisha Iran kuwafukuza raia milioni 2 wa Afghanistan waliokimbia utawala wa Taliban

Hatuna la kujadili mimi na wewe,,jielimishe hlf uje kwenye meza ya majadiliano

sawa, naheshimu maoni yako.. lakini cha kujua ni kuwa uislam ni mpango wa waarabu (pamoja na ujinga wao, hilo wamefanikiwa), kueneza mila na desturi zao kwa watu ambao hawajielewi.

lingine nenda kajielimishe kuhusu uislam ukiwa na open mind ili ufikiri nje ya box. usimeze kama dodoki
 
Nilitaka kukudharau lkn huenda nikufanyie subira kidogo kabla sijakudharau moja kwa moja

Naomba uniambie Uislamu ni nini?

Halafu nitajie nguzo tano za dini ya uislamu?

Ebu tuanzie hapa kwanza,ukiweza kujibu tutaendelea na mjadala na ukishindwa basi endelea na porojo zako kwa wadau wengine
 
Kwamba kiingereza ndiyo huelewi?

Neno 'illegal migrants hukuliona hapo? Nchi zote duniani zina sheria kali dhidi ya wahamiaji haramu.
 
Ni uislamu tu ndiyo mpango wa Waarabu kwa watu wasiojielewa ama hata ukristo ni mpango wa wazungu kwa watu wasiojielewa?
 

Teh teh teh
Hivyo vyote navijua...
Dini zote zina nguzo, na nguzo hizo siyo lazima kila mmoja akubaliane nazo.
Pia kulazimishia waumini wa uislam popote walipo duniani kufuata au kutumia lugha, majina na tamaduni za kiarabu kwa watu wengi, hilo ni doa. inaonekana dini hiyo ni kwa ajili ya watu wa jamii fulani tu, ilhali Mungu ni wa wote.
 
Ni uislamu tu ndiyo mpango wa Waarabu kwa watu wasiojielewa ama hata ukristo ni mpango wa wazungu kwa watu wasiojielewa?

Kwa upande fulani uko sahihi, Lakini ukristo haulazimishi watu wabadili majina, lugha, desturi ili kuwa wafuasi wake.
 
Huwa sipendi porojo boss

Sijakuuliza nguzo za dini nyingine kwasababu hazina misingi madhubuti,nimekuuliza nguzo za kiislamu

Ungeweza kujibu tungeendelea na mjadala na kuona kwamba uislamu si mila wala tamaduni ya waarabu

Naomba nikuache na porojo zako

Asante
 
Toka vita vianze vya Afghanistan ni Iran na Pakistan ndio wanahifadhi wakimbizi wengi kuliko yoyote so hoja yako ya Transit haina mashiko. Wakati walioanzisha vita wanachukua elfu kadhaa hao kina Iran na Pakistan wana mamiliono ya Wakimbizi.

Pia no Amount of hela inaweza kusolve hilo tatizo, Tanzania tuna wakimbizi kama laki 2 tu na bado unasikia matatizo hapa na pale, tunaongelea wakimbizi in millions hapa, hao 3.5M ni official figure za UN ila wapo kibao ambao hawana permit inakadiriwa wanaweza fika milioni 6.

Kiasi alichopokea kama mwaka jana ni kama $26M hela ya karanga hii nipigie budget yake inalisha vipi watu milioni 3.5 kwa mwaka iwapeleke hospitali na mambo mengine.
 

Duuu, hii ni ajabu na kweli. Yaani kwa uelewa wako unaona kabisa nguzo za uislamu ni imara kuliko dini nyingine. Swali dogo tu, ni chombo gani ambacho kinachoaminika kilichotoa endorsement kwamba nguzo za uislam ni thabiti.
 
Waislamu wenyewe kwa wenyewe hawapendani wao wanachojua ni kuwachukia wayahudi, wakristo na wahindi, ndiyo maana waarabu wakimbizi hawakimbilii nchi tajiri za waarabu wenzao eg Saudi Arabia, Qatar, Quwait au UAE wanakimbilia nchi za wanaoiwaita Makafiri!!
 
Sasa wanakimbia nini?
Si wamepata utawala unaoongoza kwa misingi ya dini yao pendwa?
 
Huelewi sheria za ukimbizi wewe. Mkimbizi hata akiishi hotelini kwa pesa yake, bado ni mkimbizi. Kuwa wengi haiondoi status yao, wakimbizi wanatambuliwa na UN na gharama zinalipwa na UN refugee relief, hata taifa likitumia pesa zake kusaidia zitalipwa na UN hata ikiwa baada ya miaka 100. Pia kuna mashirika mengi husaidia kugharamia huduma mbali mbali, bila kujali utajiri au umasikini wa mpokeaji wakimbizi.
Tanzania tunaweza kupokea population ya Rwanda, Burundi, DRC, Somalia, Ethiopia na kokote, lakini mashirika ya UN ndiyo hutoa usajiri na utambulisho wa wakimbizi, kisha kuanza kufanya logistic yote ya kuwahudumia. Na kufanya vetting za kuwahamisha kuwapeleka mataifa yenye uwezo kama ulaya, na America.
Huko Iran ni vituo tu, nchi husika hulipwa kuhudumia.
Nenda Ngara na Kibondo kajifunze.
 
Boss nishakutajia Amount ilioenda kule, ni dola milioni 20 na kitu tu nipigie hesabu inahudumia vipi hao wakimbizi?

Hii article ya UN wenyewe

Kiasi kilichotakiwa kiende ni 114M na kilichoenda ni asilimia 23 tu.

Pia for the sake of discussing assume UN wamelipa hela yote hio dola milioni 114 fanya hesabu rahisi

114M gawanya kwa 3.5M unapata hapo unapata 32 dollar.

So mkuu nipigie hesabu kumhudumia mkimbizi mwaka mzima kwa dola 32 unawezaje? Hio ni sawa na hela za madafu kama sh 200 kwa siku hata chapati hupati unamhudumiaje?

Iran inasomesha watoto wakimbizi 800,000 shule za Iran wanakaa na watoto wa Iran wanachanganyika, sio gharama za Kitoto mkuu.
 
Kwani wewe unampenda Mama Samia?
 
Waswahili bana mnachekesha!
France, Germany kuwafukuza wahamiaji toka West and North Africa umewahi lizungumzia!?
 
Hao waarabu mila zao haswa zinapingana na uislam.
Unajua mila haswa za waarabu!?
Tuanze kuzijadili na tuzifanananishe na uislam kama zinafanana!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…