INASIKITISHA: Makaburi Kinondoni yanavunjwa makusudi ili ipatikane nafasi ya kuzikia

INASIKITISHA: Makaburi Kinondoni yanavunjwa makusudi ili ipatikane nafasi ya kuzikia

Kaburi likiwa limevunjwa na linaendelea kusambaratishwa. View attachment 1937397
mimi nashangaa manispaa ya kinondoni kwanini hawakatazi watu kuendelea kuzikana pale maana kumejaa sna na mateja wapo pale ndio wanaofanya huu ujinga wanatafuta makabuli ya mda kidgo wanayaharibu makusudi hii si sawa ni lazima tuwaheshimu ndugu zetu walitangulia mbele ya haki kama kumbukumbu kwetu na ndugu zao..serikali mnasubili nini kuzuia huu ushenzi unaofanyika hapo kinondoni?
update ..
nimepita hapo mda huu ni kweli kabisa nimeshuhudia hayaa kwa macho yangu wahuni tu wapo pale wanatafutatafuta visehemu wanachimba kwa kuharibu makaburi ya zamani. hii si haki.
 
Unatembelea kaburi ili upate nini
Wengine wanatembelea makabuli kwa ajili ya ibada kulingana na imani zao zinaruhusu wengine wanatembelea makaburi kama sehemu ya kumbukumbu ya ndugu zao walitangulia mbele ya haki.. Swali kwako wewe mwenzetu mkisha zika huwa amgeuki nyuma au huwa hata hamziki mnatupa tu maiti..
 
Angalia wasituharibie hili
20210914_163409.jpg
 
Hapo kinachofanyika ni uhuni wa daraja la juu. Tulinunua eneo la kuzikia sh millioni 2, tukaambiwa tulipe laki 3 ya wachimbaji. Aisee kwenye kaburi la ndugu yangu ilifukuliwa mifupa ya mtu aliyezikwa zamani. Tukiwa tunazika, wachimbaji wakaomba waifukie mifupa ya yule marehemu wa Kwanza mle kaburini
 
Kujengea makaburi mi naona si vizuri imagine mababu zetu wangekuwa wanajengaga makaburi Leo tusingepata sehemu aisee
Watu sema hawasomi Historia hii tabia ya kujengea makaburi imekuja kupelekea watu wanayaabudia makaburi.

Kiasili ni kuweka alama na ikipita miaka mingi sehemu hiyo waje wazikwe na wengine.

Huku kwetu kujengea makaburi ni HARAMU na kufanya hivyo unapata madhambi.
 
Makaburi hayatakiwi kujengewa ili baada ya muda watu wengine wapate nafas ya kuzikwa sasa unajengea ili watu wengne wakazikwe wap? Dawa ni kuyabomoa kabisa sawazisha eneo miaka 30 ijayo watu waendelee kuzikwa hapohapo

Mababu zetu wangekua wanayajengea tangu enzi hizo sahivi kila sehem kungekua na makaburi Nawapongeza wanaofanya ubomoaji huo.
 
Hapo kinachofanyika ni uhuni wa daraja la juu. Tulinunua eneo la kuzikia sh millioni 2, tukaambiwa tulipe laki 3 ya wachimbaji. Aisee kwenye kaburi la ndugu yangu ilifukuliwa mifupa ya mtu aliyezikwa zamani. Tukiwa tunazika, wachimbaji wakaomba waifukie mifupa ya yule marehemu wa Kwanza mle kaburini
[emoji24][emoji24]
 
Sasa huu ni ujinga ulio pea.

Kumbukumbu si lazima ujengee,ukiweka alama inatosha.

Nimekupat.
Anayehusudu tambiko ni Kissendi Nyanda Ntalima Mpandagoya.

Yaani eti kweli Teja akifa anaweza kukupa utajiri ukimuomba?

Maana Teja naye hugeuka mzimu
 
Ila sisi binadamu tuna uchuro sana. Kwanini ujengee kaburi? Tena ikiwa ni makaburi ya public?

Kama ni makaburi ya familia sawa jengeeni ila kama unazikwa kwenye cemetery za jumuiya msiwe mnajengea. Kwasababu kiuhalisia ni kuwa ingekuwa makaburi hayafukuliwi na kuzikwa wengine hapo Kinondoni pangeshajaa miaka ya zamani sana.

Wanaojengea makaburi ni wabinafsi tu. Mtu akishakufa amaekufa mzikeni sawa ila msijengee kaburi ili na wengine wakifa wapate pakusitiriwa.

Ifikie mahali pia tuwe na tamaduni za kufanya cremation (kuchoma miili baada ya taratibu za msiba). Hii itapunguza uhitaji wa ardhi ya kuzikia watu.

Sisi wamasai zamani mtu alikuwa akifa tunampaka mafuta ya kondoo na anapelekwa vichakani huko analiwa na fisi habari yake inakuwa imeisha.
 
Ila sisi binadamu tuna uchuro sana. Kwanini ujengee kaburi? Tena ikiwa ni makaburi ya public?

Kama ni makaburi ya familia sawa jengeeni ila kama unazikwa kwenye cemetery za jumuiya msiwe mnajengea. Kwasababu kiuhalisia ni kuwa ingekuwa makaburi hayafukuliwi na kuzikwa wengine hapo Kinondoni pangeshajaa miaka ya zamani sana.

Wanaojengea makaburi ni wabinafsi tu. Mtu akishakufa amaekufa mzikeni sawa ila msijengee kaburi ili na wengine wakifa wapate pakusitiriwa.

Ifikie mahali pia tuwe na tamadani za kufanya cremation (kuchoma miili baada ya taratibu za msiba). Hii itapunguza uhitaji wa ardhi ya kuzikia watu.

Sisi wamasai zamani mtu alikuwa akifa tunampaka mafuta ya kondoo na anapelekwa vichakani huko analiwa na fisi habari yakw inakuwa imeisha.
True
 
Back
Top Bottom