Inasikitisha na kustua sana. Marehemu Kambayao wa TRA alikuwa pia Mwanachuo CBE Dodoma

WAnadeal na matokeo siyo chanzo... hii haiwaondolei hofu wananchi kwa sasa kuogopa watu wanaokuja kama polisi au tra kwa sababu toka mwanzo watu wanatekwa na hakuna aliyekamatwa kwa utekaji. Haya ndiyo matokeo yake sasa.
Solution ni kutafuta mzizi wa chanzo kwanini iwe zama hizi na si zama nyingine yoyote?
 


Tulisha waambia msipuuze tekateka sasa mnaona wenyewe. Hapa mbona bado hakuna aliye salama hata wewe hauko salama
 

Wakija wasiojulikana wenyewe mitanganyika inajificha. Hovyo sana
 
Hakuna bachelor degree ya part-time.
 
Wakija wasiojulikana wenyewe mitanganyika inajificha. Hovyo sana
Unatofautisha vipi wasiojulikana na vyombo vya usalama? Maana mara zote unasikia wanasema alichukuliwa na waliodai ni polisi walikuja na landcruiser.
Sasa hiyo hali ya kutoweza kuwatofautisha ndiyo inawafanya watu wawe na mashaka na kila anayejiita TRA, polisi. yani sasa hivi ukisikia mtu kafuatwa na polisi unadhani kaenda kufa tofauti na zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…