Huyu siyo Rais wa jamhuri.Uliona wapi Rais wa jamhuri anahamasisha ufisadi katika Taifa?!Unakosea sana bwana mdogo
View attachment 2187306
Usiitweze ubinadamu wa mtu yeyote.
Mwanadamu mwenzako huwezi kumwita majina ya ajabu. Kila mmoja alijua Magufuli alikuwa dikteta, mtekaji, mpotezaji na muuaji wa wqtu aliotofautiana, alikuwa na upeo duni wa masuala ya uchumi, biashara na mahusiano ya kimataifa. Hata hivyo, bado kutokana na ubinadaku wake, hakuma aliyemwita kwa majina hayo uliyoyatumia dhidi ya Samia.
Sijawahi kuwa shabiki wa mtu, na sitakuwa, lakini hata katika kutofautiana, tusiutweze ubinadamu. Tunajua Magufuli alipora uchaguzi. Na ni uchaguzi huo huo ndio unaomfanya Samia awe Rais leo, lakini je, tumkatae kwa sababu ni zao la uchaguzi batili? Ukifanya hivyo, utarekebisha vipi makosa na ujbazi wote uliofanyika kwa miaka karibia 6?
Tukubali kuwa Samia ndiye Rais, tushirikiane naye kuleta mabadiliko. Asipotoa ushirikiano kwa wananchi, tumshinikize, lakini siyo kumkataa kwa namna yoyote ile. Kuna nchi, marais huingia kwa mapinduzi. Nani anakuwa amemchagua? Lakini si anajulikana kuwa ni Rais? Na anakuwa na nguvu zote?
Rais Samia, bila ya kujali ameingiaje, cha muhimu asimamie mageuzi makubwa yanayotakiwa kwa nchi yetu.