Inatosha ndugu yangu; Mshukuru Mungu kwa yote, rudisha vitabu kwa Mkuu wa shule, chukua jembe itafute njia ya Nanjilinji ukajilimie ufuta!

Inatosha ndugu yangu; Mshukuru Mungu kwa yote, rudisha vitabu kwa Mkuu wa shule, chukua jembe itafute njia ya Nanjilinji ukajilimie ufuta!

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Ulitoka makao makuu yetu ya wilaya kwenda huko mbali kisiwani kwa ajili ya kujitolea na umekuwa ukijitolea kuwasaidia watoto hawa eneo hili la kisiwa lenye changamoto ya elimu na linaloogopwa na kukimbiwa na watu kila siku kwa juhudi zote tangu 2018....
somo lako ulilopewa, linaloaminika kuwa ni gumu kuliko yote (ndivyo ilivyo akilini mwa wanafunzi wote, kutoka primary hadi vyuo), ukalisimamia vema na likaongoza katika ufaulu wa darasa la saba katika shule hiyo na za nyiiingi zingine.
nidhamu ya kazi unayo vema kwa uliowakuta wote mpaka wakakuona sehemu yao na kutotamani utoke

Ajira za 2018 zikatoka nawe HUKUWEMO.....ukaendelea na kazi bila kinyongo.

2019, kwa mara nyingine tena, somo lako kwa darasa la saba likafanya vizuri sana. Shule na jamii nzima wakatambua pasipo na shaka uwezo na jitihada zako katika kuwapigania watoto wetu. Kuanzia hapo, hakuna kambi za pamoja zilizowekwa we ukakosa kutakiwa kuwepo........umelala chini, umekula vyakula vya wanafunzi, umekesha na kuamka asubuhi sana kwa ajili ya watoto hawa wa kitanzania. Ulifanya hayo huku ukijua fika kuwa si muajiriwa, hauna mshahara!

Ajira chache za 2019 zilitoka nawe HAKUWEMO.

2020 Moto wako wa kujitolea ukawa uleulena na kama 2019, ulikesha katika makambi kuwasaidia vijana na safari hii ukahusika kwa kiasi kikubwa kuifanya shule kushika namba moja wilayani kwenu......zawadi zilitolewa, nawe umetambulika kwa mchango.

Zilipotoka ajira za 2020 HUKUWEMO!

2021 ukaendelea tena kujitolea kwa kasi ya ajabu, huku walimu walioajiriwa na watu wengine wakianza kukushangaa, 'kwani huyu vipi mbona hakomi tu?!!!! Future yake n nini?!!' Tena, matokeo ya somo lako na shule yalikuwa bomba kupindukia.

Ajira za 2021 zilitoka nawe HAUKUWEMO!

Ukaendelea kujitolea bila kujali kukosa kwako ajira au dhihaka za walimu waajiriwa wasiowajibika sawasawa na wasiowahi kupara jeraha hivyo hucheka tu kila walionapo kovu. Watoto wakaendelea kuelewa, wakafurahia uwepo wako.

Zikatoka ajira 'kiduuuuchu' sana mwanzoni mwa 2022, kama za watu 150 hivi, wewe HAUKUWEMO.

Ukaendelea kujipa moyo huku ukiendelea kujitolea kuwa safari hii, kutokana na ahadi ya mama Samia ya kumwaga ajira zaidi ya 9000, inawezekana ukakumbukwa.

Ndg yangu, leo napata orodha hii iliyotolewa na serikali ya ajira za walimu walioajiriwa mwezi huu wa juni, HAUMO! Nimetafuta mara kutafuta jina lako ili niamini na sasa nimeamini kuwa ni kweli HAUMO!

Ndugu chukua jembe na shoka nenda zako Nanjilinji ukajilimie, huku si kwako, HAUTAKIWI. Sina uhakika kama huko pia kunakutaka lakini utajua ukifika, huku imeshajulikana.

Uwepo wa waliomaliza hadi 2020, muda ambao wewe unajitolea kwa mwaka wa tatu mfululizo, ni ishara ya wazi kabisa kuwa huku HAUTAKIWI, pengine kuna wenyewe lakini kwa sababu mi sijui basi nasema tu kuwa HAUTAKIWI huku.

Nenda Nanjilinji ndg yangu kaitafute amani ya moyo, najua umefadhaika kiasi gani hapo ulipo sasa lakini ndo maisha....nenda Nanjilinji, kuna sauti inaniambia hivyo. Utapata amani ya moyo huko na utasahau yote na kushukuru hata kwa haya maisha tu. Tahadhali, nazungumzia amani ya moyo na si utajiri....hakuna utajiri katika jembe la mkono!

Najua hauna hata mia, lakini nenda kwa furaha ndugu yangu....miaka yako mitano ya kujitolea bure ni jambo kubwa sana. Wale watoto uliowapatisha A na sasa wako vipaji maalumu; kilakala, kibaha, nzumbe na wengine iliboru nina uhakika watakukumbuka sana....na hilo ni jambo jema.

Jamii ya hapo unapojitolea duwa zao zi pamoja nawe, hilo nina uhakika kabisa. Ukweli ni kuwa wanakuhusudu sana. Tena ulivyo na adabu uliamua kuposa binti yao na hatimae kufunga nae ndoa bila kuleta uhuni wowote.......wazazi wetu, hawakuamini jinsi ndoa yako ilivyowezeshwa na jamii ya hapo; michango ile ya vitenge, kanga na mashuka ni ushahidi tosha kuwa umeishi nao vizuri sana. Hawa wanakuzungumzia vizuri sana na wapo pamoja nawe kwani wameona uliyoyafanya kwa watoto.

Kajifiche Nanjilinji ndugu yangu, uonekano wako kwa sasa unaweza kuwatisha na kuwakatisha tamaa wanaosoma na wanaofikiria kujitolea......hawa hawajui kuwa una nuksi tu na HAUTAKIWI bali watafikiri kuwa hakuna ajira. Zipo ila si kwa wewe.

Umri unakwenda ndugu yangu nenda kajifiche Nanjilinji, ndg zako waliomaliza mwaka 2020 2019 na 2021 na sasa kuajiriwa watakukuta na kukushangaa......si vema katika umri huo kugeuka kuwa 'laughing stock'!

Pole sana na kila kheir ndg yangu.......
 
Elimu tuelimishe na sisi tufanikiwe, maneno ya wazee hayo.



Kukuuuu [emoji239][emoji239][emoji239]
 
Kwani hatima ya Maisha ya Mtu Ni Kupata Ajira ya ualimu this is pathetic

Kama kujitolea kunalipa ...just do it kila Mtu afanye anachopenda that way tunaishi only once.
 
It's very touching in deed. Ila hawa ndio hufanya serikali ione hakuna uhaba.
 
Back
Top Bottom