Heri angegombea mbowe mwenyewe maana alichokifanya Tundu ni sawa alikuta chama kinapumulia mashine yeye akakikatia kabisa na kukiingiza kaburini
Nadhani hili litakua fundisho kwa wapinzani wa vizazi vijavyo
Hata mimi Tundu aliporudi na kuanza kutema nyongo binafsi, niliwaza ni bora Mbowe angesimama mwenyewe, maana mengi yalimkuta awamu hii angeweza kuyaunganisha na sera.
Shida Lissu alishatangaza tangu ile enzi ya HARDTALK BBC kuwa atarudi kugombea uraisi.
Chadema nadhani walijua sio mtu sahihi ila hawakuwa na uthubutu wakumwambia sababu ya:
(1.) ubabe wake,
(2.) Kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza anarudi tangu Lissu ale shaba, walidhani watu watakuwa na huruma naye (kumbe watu wanapambana na hali zao,
(3.) ACT-WAZALENDO walikuwa hawana mgombea kipindi hicho, na Zitto amekuwa akijifanya BFF wa TL tangu shaba, hivyo walihofia TL kujiunga naye na kuiua CHADEMA.
Ukiangalia kampeni za TL mwanzoni akiwa na Mwamba, utaona Mwamba alikuwa hana amani. Na kibaya zaidi TL alitumia kampeni zile kumwaga nyongo binafsi badala ya kuuza chama au sera.
Ila wasivunjike moyo.
Mwamba arudi to basics. Atafute damu mpya, yenye akili zilizotulia kama akina Dr. Slaa waisuke Chadema upya. Waachane na siasa za kiki, zimepitwa na wakati. Aachane na baadhi ya wakongwe wanaofanya siasa kwa mazoea na hawataki kubadilika. Aone Magu alivyoibadilisha CCM, nayeye anaweza kuibadilisha Chadema.