Inauma sana, wezi walaaniwe. Wamenirudisha nyuma sana

Pole sana sana, naelewa unachisema na kukiptia Mwezi wa nane tarehe 15 walinifanyia ukatili huo, waliniibia Laptop na simu mbili, wala simu sio tatizo lakini Laptop ilikua na DOCUMENTS muhimu sana snaa, miongoni mwa documents hizo ni Consultancy ambayo nilikua nimeshamaliza Inception Report, Desk Review na nilikua namalizia kuandaa tools kwa ajili ya data collection. Kinachoniuma ni kwamba hizi ndio deliverable zinazonifanya nilipwe, yaani una/submit unalipwa per deliverable....nilitamani dunia isimame. Yaani nadaiwa kazi ya watu na sina hata pa kuanzia tena......Pole sana sana
 
Pole sana mkuu, ni wengi tumeumizwa na wezi, mwenyewe nimetoka kuibiwa mwezi uliopita na nikaripoti polisi hakuna msaada wowote!
Ahsante na pole pia, polisi hao sitaki hata kuwasikia kwanza watakuzungusha tu nakukuzidishia maumivu. Nilijifunza kipindi Mdada alivyotapeliwa.Wale matapeli walimuachia smartphone. Nikaripoti polisi wakaichukua ile simu na sikuipata hadi Leo hii na hakuna chochote kilichofanyika zaidi njoo kesho njoo kesho hadi nikakata tamaa.Afadhali wangenipatia ile simu ingepunguza hasara kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…