Inaumiza sana kuona wa Africa wanatetea dini kuliko rasilimali zao

Inaumiza sana kuona wa Africa wanatetea dini kuliko rasilimali zao

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,646
Reaction score
36,604
Inaumiza sana kuona wa Africa wanatetea dini kuliko rasilimali zao, hata baada ya kuwafukuza wakoloni Africa bado tunawapelekea wakoloni hao hao rasilimali fedha ambazo tunachangishana makanisan sadaka na misikitini (hija fee).

Yaani hela zetu zinawafikia wakoloni wakiwa wamekaa, mtaji wao ni biblia na Quran tu.

Jiulize kabla ya dini za wakoloni kuja africa, je africa kulikuwa na shetani?
 
MTU ANAKUAMBIA UKIUA MWENZAKO BASI UTAZAWADIWA KUNDI LA WANAWAKE LA KUFANYA NALO MAPENZI NA MIFEREJI YA POMBE ZA BURE
Screenshot_20261029_172512_X.jpg
 
Inaumiza sana kuona wa Africa wanatetea dini kuliko rasilimali zao, hata baada ya kuwafukuza wakoloni Africa bado tunawapelekea wakoloni hao hao rasilimali fedha ambazo tunachangishana makanisan sadaka na misikitini (hija fee).

Yaani hela zetu zinawafikia wakoloni wakiwa wamekaa, mtaji wao ni biblia na Quran tu.

Jiulize kabla ya dini za wakoloni kuja africa, je africa kulikuwa na shetani?
Hapa unaandika jpili waenda kanisani kama kawa
 
Shetani yupo sku zote ata wazee wetu walikua wakiomba mizimu pale kunapokua na tatizo au shida fla
Iyo shida au tatizo flan ndo shetani uyo.

Mvua hazinyeshi wazee walikua wanaomba na kujiuliza wamewakosea nn mizimu sasa iyo mizimu ilikua iko mara mbili kuna mizimu mema(miungu) na kuna mizimu mibaya (shetan)
 
Mimi ninadhani mabadiliko yaanze na sisi kwa sababu kama ni ujinga mababu zetu wengi wao walikuwa wajinga kwelikweli. Jiulize wakati mzungu anajenga Titanic mwanzoni mwa 1900 sisi mababu zetu walikuwa wanafanya nini? Mizimu nayo ilishindwa kabisa kusaidia mababu kupata akili za kufanya mambo makubwa kama watu wa Ulaya, America na Asia. Lakini hata kwa nyakati hizi bado hali ni mbaya. Kwa mfano mtu anayeambiwa na Mwamposa pokea muujiza wako wa nyumba na gari ataweza kufikiria jambo lolote kubwa?
 
Back
Top Bottom