Artificial Horizon
JF-Expert Member
- Jul 31, 2019
- 432
- 977
Wakati wa Mungu ni sahihi kila kitu kitakuwa sawa.
Sema lazima upambane na hili suala la ajira ni Karibu Afrika yote.
Sema lazima upambane na hili suala la ajira ni Karibu Afrika yote.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani huko ulaya mifumo yao ya elimu ndio imekaa kimfumo wa kujiajiri..?Education system inatugharimu San nchi nyingi za Africa,,
Elimu imekaa katika mifumo ya kuajiriwa siyo kujiajiri
Naomba posts kama hizi kabla hujafika mbali muwe mnatuambia na nyie mlianzaje maisha ,,, mfano elimu ya awali DiplomaINAUMIZA SANA KWA KWELI UNAPOONA WASOMI WAZURI ILA WANA HALI NGUMU KIUCHUMI.
Ukiwaambia ,wanakwambia graduates wavivu .Kwani huko ulaya mifumo yao ya elimu ndio imekaa kimfumo wa kujiajiri..?
Cha msingi serikali ifanye wajibu wake wa kuhakikisha kunakuwa na fursa nyingi za ajira na kujiajiri kwa vijana na sio siasa au propaganda kila sehemu.
Hawa European na USA au China na japan sio wajinga wanakuwa na data za kila mwezi kuhusu hali ya ajira ya wananchi wao..
Haiwezekani wanatoka vijana wenzetu hapa hawana ajira wanafika ulaya na america wanapata ajira on spot na wanaanza kuwekeza huku kwa nn sisi tunashindwa tunashida mahali ise.
Mimi nilishaacha huu ujinga.INAUMIZA SANA KWA KWELI UNAPOONA WASOMI WAZURI ILA WANA HALI NGUMU KIUCHUMI.
Wazazi tuchukue tahadhari, Tusomeshe watoto sambamba na kuwaandaa waweze kujiajiri ama kufanya biashara, degree/masters zinawaaibisha watu mitaani
Wazazi tunapaswa tubadilike sana kwenye kuwekeza kwa ajili ya watoto wetu. tuwekeze kwenye mali zaidi kuliko kuwalipia ada mamilioni mwisho wa siku wanarudi nyumbani wakiwa hawawezi hata kujitegemea
Na wale wa bussness adminstration na Commerce vipi?Acha huyo mzee, kuna mshikaji wangu amesomea "MIPANGO" ana degree ya Mipango na hela hana!
Sasa sijui kasoma mipango gani?
Huwa namuuliza hata yeye hana majibu.
Ule ujiko wa kusoma kama huna hela hauna maana tena.Hayo ndo mapambano yenyewe mkuu. Usishangae hadi huku vijijini kwetu sasa vijana wasomi wapo na kazi inaendelea boda, kilimo, ufugaji, mikopo/ujasiriamali, saidia fundi, migahawa etc. (Hoja ya kiwango cha elimu wameiweka pembeni kwanza - wanapiga kazi).
Cha msingi ni wajipatie riziki kiHalali na wasikalie kazi ya kulalamika kutwa nzima as if kuna mtu amezuia au amehodhi nafasi za ajira kiasi kwamba ndo imesababisha wao wasipate au wakose ajira.
Kabisa mkuu.Ule ujiko wa kusoma kama huna hela hauna maana tena.
Cha msingi kila mtu mkono uende kinywani.
Hakuna kitu kibaya kama kuwa Broke hadi mla unakuwa wa taabu.

Ni kweli mkuu, lakini inakuwa kwanza mtoto au mjukuu yeye mwenyewe aoneshe kwamba anaihitaji hiyo nyumba ila anashindwa uwezo. Mtoto kuwa utingo wa mafuso yao nyumbani (kama mtihani kwake) ni sawa ili ajifunze, apate uzoefu na mwisho kama akionesha kweli anamudu shughuli hiyo na ameipenda, akipewa fuso lake ili sasa yeye ndo awe mmiliki wa mali hiyo au ni dereva au msimamizi, mfuatiliaji na mkusanayaji mapato ambayo ni mali yake, hiyo ni sawa. Vinginevyo tofauti na hapo, hilo fuso linaweza kuwa ndo mwisho wa maisha yake. Ukimjengea nyumba anaweza kuitelekeza hapo na akaishia kusikojulikana.Mkuu kila mtu ana namna yake ya malezi. Wapo wanaojenga nyumba hadi za wajukuu na wapo ambao hawawapeleki shule kusoma degree. Kuna mzee mtoto akimaliza form four anakuwa utingo wa mafuso yao ya nyumbani akizoea anapewa fuso lake aanze mapambano. Na wote wapo vizuri.
Ni kweli na maumivu yake yanawapata pia hata wazazi kwani wote wazazi na watoto walichotegemea kuwa ndo yatakuwa matokeo ya usomi imekuwa ni kinyume chake.Huu uzi una utani wa kweli, unauma huoo.
Mkuu kama unaweza, mali kwa uzao wako ni lazima si suala la uhitaji wa mtoto. Hata kama kasoma, kumpatia kiwanja, nyumba akiwa anaanza maisha ni sahihi. Ile inarahisisha mambo mengi na kuondoa vizazi vyako katika umasikini. Kama inawezekana lakini ila kama huwezi unafanya lile linalowezekana ila hakikisha mwanao hapitii yale uliyopitia, njia yake iwe na unafuu.Ni kweli mkuu, lakini inakuwa kwanza mtoto au mjukuu yeye mwenyewe aoneshe kwamba anaihitaji hiyo nyumba ila anashindwa uwezo.
Yataka moyo na mtu ajipange vizuri tokea wanawe wakingali wadogo. Ipo mifano mingi (nadhani unaijua hata ww) ya matajiri waliojaribu hivyo lakini mara tu baada ya kifo chao, kulianza mtifuano ndani ya familia wakigombea mali alizoacha marehemu hata kama aliandika wosia. Wengine wamediriki hata kuuana katika ugomvi huo.Mkuu kama unaweza, mali kwa uzao wako ni lazima si suala la uhitaji wa mtoto. Hata kama kasoma, kumpatia kiwanja, nyumba akiwa anaanza maisha ni sahihi. Ile inarahisisha mambo mengi na kuondoa vizazi vyako katika umasikini. Kama inawezekana lakini ila kama huwezi unafanya lile linalowezekana ila hakikisha mwanao hapitii yale uliyopitia, njia yake iwe na unafuu.
Unajua kwanini wapo wanasiasa hawashibi na wanajua hawaishi milele? Wanataka kuacha urithi hadi wa vitukuu.
Huu mfumo haufai kutumika kama una watoto wa mama tofauti tofauti unless ulitumia nafasi yako kama baba kuwaleta pamoja wakawa kitu kimoja, yaani watoto wapendane bila kujali mama zao wanawaambia nini.Yataka moyo na mtu ajipange vizuri tokea wanawe wakingali wadogo. Ipo mifano mingi (nadhani unaijua hata ww) ya matajiri waliojaribu hivyo lakini mara tu baada ya kifo chao, kulianza mtifuano ndani ya familia wakigombea mali alizoacha marehemu hata kama aliandika wosia. Wengine wamediriki hata kuuana katika ugomvi huo.
Ngozi na rangi yake visisingiziwe.Ni kawaida mtu mwenye ngozi nyeusi akiwa na uhakika wa kula na kulala kumuona asiye na uhakika wa kula na kulala ni mvivu na mzembe.
Hii ngozi ni kama ina laana.