Inawezekana Freeman Mbowe ndiye aliahidiwa kupewa Ubunge wa kuteuliwa ili CHADEMA isimsumbue Rais Samia?



Ubunge utamsaidia nini mtu ambaye ni billionea !
 
Wewe
Mpaka Dkt Nchimbi anawaombea huruma "makosa madogo madogo" Mbowe yupo kimyaaa. Wewe unadhani ni kawaida?
 
Mbowe must go
 
Haya maridhiano yalikuwa hadaa tu, tatizo CDM hawakutaka kujifunza kwa maridhiano ya Ccm na Seif kule Zanzibar na matokeo yake yaliishia wapi.

Allen Kilewella econonist Nguruvi3 brazaj Kalamu
 
Figga nakuamini ujue.

Siku hizi hata baba anaweza kuisaliti familia kwa maslahi ya mchepuko
Mkuu 'Msanii', ninajisikia hovyo sana kushindwa kukupa jibu nililo ahidi kuhusu yale maneno uliyo nikumbusha juu yake. Najuwa unakumbuka.

Nimetafuta bila mafanikio ile hotuba ya Mbowe iliyo nifanya niandike maneno hayo ambayo hadi sasa yanacheza akilini mwangu na kunichafua roho.

Lakini, hatimaye, sasa (leo) tupo hapa, na Tundu Lissu kazidi kufungua pazia kusema yale yale tuliyo wahi kuyasema mara nyingi tu kuhusu Mbowe, na anako ipeleka CHADEMA. Rekodi yetu ipo wazi kabisa humu JF. Hatujayasema haya aliyo sema Tundu Lissu, mara moja au mara mbili; tumeyasema haya mara nyingi sana humu humu JF.

Sasa sijui nieleze vipi nilivyo taka kukujibu kwenye yale maneno ambayo ni kama ulinifunga mnyororo mguuni na kushindwa kabisa kujitetea juu yake.

Namshukuru sana ndugu Lissu kuniondoa wasiwasi kidogo nilio kuwa nimebaki nao kuhusu haya yaliyo jifunua sasa hivi.
 
Kunywa maji kijana wangu.
nasikitika kuyasema haya, lakini 'Retired' anapoteza hadhi yake na kupelekea aonekane kutokuwa tofauti na watu kama Lucas Mwashambwa walivyo kwa Samia.
Inasikitisha sana, kwani anaonekana kuwa na uelewa mzuri wa mambo kuliko hao wengine.
 
Ni Mbowe ndio alipewa hizo ahadi hewa, ndio maana siku moja kwenye mkutano wa cdm akawa analeta swaga za kumtetea mama Samia, huku akiwa amelewa chakari. Nadhani ndio alikuwa na hilo fungu la hadaa.
Lakini tusimnyime sifa yake pia huyo mwingine. Samia ni mzuri sana kwenye udanganyifu. Hata Magufuli alishindwa kabisa kugundua udanganyifu mkubwa alio nao huyu mama. Nadhani hizo Ph.D. nyingi anazo tunukiwa zitakuwa zinahusiana na uwezo wake wa kudanganya watu.
 
Nijuacho Mh Mbowe Hana Bei.

Tajiri kununulika Si Rahisi kama maskini.
Lakini anaweza kununulika kwa sababu nyingi nginezo, hata kama siyo sababu ya esa.
Mi naamini Mbowe ananunulika sana!
Hali hiyo ime kwisha jidhihirisha mara kadhaa wakati wa uongozi wake wa CHADEMA.
 
..mbowe amenunuliwa na nani?

..hao waliomnunua mbowe, wametoa wapi fedha?

..je, waliomnunua mbowe, hawajahongwa, au kununuliwa na wengine?

..je, mbowe ndiye mpinzani wa kwanza kununuliwa?

..kwanini hatukerwi, au kushughulishwa, na waliomnunua mbowe, na wapinzani wengine kabla yake?
 
Jamani tatizo nini, mbona kuna wanaume wengi tu wanatongozwa na wanawake siku hizi?kama alitongozwa akapewa ahadi za uhongo na baadaye ikaja kujulikana alikubali kudanganywa, tatizo ni la SSH au la huyo Chairman?
 
Kama Mbowe ana'hongeka na Lissu nae ni walewale "wamepishana kwenye maslahi"
Mungu tunusuru
 
Mkuu Kalamu
Kuwa na amani sana. Huu mjadala umepanuka sana mpaka sasa.

Wasaliti wa movement wataelea kama mafuta juu ya maji
 
Erythrocyte una la kuongeza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…