Inawezekana kipindi cha Mkapa ndio ujambazi mkubwa ulitamalaki

Inawezekana kipindi cha Mkapa ndio ujambazi mkubwa ulitamalaki

Kwa tukio la NMB Ubungo Mataa inasemekana kuna silaha ya kivita iliazimwa kutoka kambi moja wapo ya Jeshi.

Source: Kijiwe cha gahawa..
Umenikumbisha hili tukio lilipangwa vizuri mnoo yani moja kati ya misheni iliyokaa kibabe sana.... Harafu jamaa walijua plan b ilienda vizuri maana mpka watuhumiwa walikamatwa na sio wahusika hawakuiba ile mtu unafanana nae unamuweka kwenye target anajua ndo plan b na ushahidi woteee jamaa mmoja alikamatwa kinondoni mchana kweupe anakula ugali na mke wake alikaa jela miaka kumi na tano.....
Badae sana kundi lile likafanya ambush mmoja akakamatwa baada ya mateso makali akataja mnyororo wote ndio kilichomsaidia bwana aliekamatwa kinondoni kutoka. Alitoka akili ikiwa imeharibika vibaya mno na bahati mbaya alifariki.
Hii ni chai ya mlevi
 
Mwaka 2004 pale Sanawari walipora kwenye kontena la Voda na kumuua mtoto aliyekuwa anapita zake. Mhudumu alijeruhiwa na risasi. Toka hiyo siku nilisapoti sana jambazi likiuwawa. Kifo cha mtoto kiliwauma wengi. Magu alifyeka sana majambazi na vibaka. Vijana wahuni wengi wa Mburahati na Kigogo walikimbilia South Africa
 
Kuna
Mwaka 2004 pale Sanawari walipora kwenye kontena la Voda na kumuua mtoto aliyekuwa anapita zake. Mhudumu alijeruhiwa na risasi. Toka hiyo siku nilisapoti sana jambazi likiuwawa. Kifo cha mtoto kiliwauma wengi. Magu alifyeka sana majambazi na vibaka. Vijana wahuni wengi wa Mburahati na Kigogo walikimbilia South Africa
Kuna jamaa alikuwa na bureau de change pale namanga hatua chache kabisa na Oyster bay polise walimuua Dec 24 asubuhi
 
Bwana jiwe aliukomesha
Na alitangaza hadharani, majambazi wanyang'anywe silaha harakaharaka. Alitoa ile kauli kimzahamzaha ila kumbe alimaanisha.

Baada ya hapo stori zikawa ni mwndo wa majambazi yauawa wakati yakijaribu kupambana na polisi. Yani kama wewe ni jambazi unawekwa kwenye rada, unakamatwa unapelekwa milimani/maporini unapigwa shaba kisha asubuhi na mapema unakuwa kwa niuuuuz
 
Baada ya matukio ya uvamizi kushika kasi ndio ikaja sheria mpya ya askari kulinda vituo kuweka uzio na vizuizi na raia kutoruhusiwa kuingia na gari hasa nyakati za usiku.. Na baadhi ya vituo vikawa vinafungwa usiku
Sidhani kama hii nchi imewahi kuwaogopa wahalifu kiasi hicho....
 
nasikia watuhumiwa wengi walikua wanatoka mara serikali ikatumia njia ya kuwapa kipaumbele jeshini na upolisi sasa ivi hali ikawa shwari.

ukichunguza ni kama kweli 70% ya polisi na wanajeshi ni watu wenye vina saba vya mkoa wa mara
Chai.

Sababu ya watu wa mara kuwa jeshini kwa wingi ni ari na ujasiri wa kupigna vita wakati wa vita ya kagera. Wakati mikoa mingine wakiwa wamelegea na wengine kukimbia kwenda jeshini, mkoa wa Mara ulionekana kama vile nafasi zilizotoleww zilikuwa kidogo kulinganisha na wanaojiandikisha. Vijana wengine wakawa wanawahi kwenda mikoa ambayo vijana wanasitasita kujiandikisha. Mwisho wa usaili ikaonekana vijana wa Mara ni wengi sana. Kuna stori ambayo in uhakika kama ni kweli ila wanasema ilibidi hata serikali iangalie nafasi za mikoa ambayo hawakujiandikisha wa kutosha, zipelekwe mkoani Mara kwasababu kule vijana walikuwa wanapambana kujiandikisha.
 
Back
Top Bottom