Pombe siyo dhambi, kosa lake nini hadi umwadhibu?
Siyo jukumu la mwanadamu "kuadhibu" dhambi!
Jitihada zinazofanyika ni kwa ajili ya kumsaidia. Uraibu ni ugonjwa mbaya sana. Fikiria:
1. Mtu ana Elimu ya Chuo Kikuu lakini hawezi kufanya kazi kwa sababu ya pombe
2. Mtu hana kazi inayomwingizia kipato lakini Asubuhi unamkuta ameshalewa
4. Mtu bado kijana lakini tembea yake ni kama anakokota miguu
5. Kutokana na pombe kukolea kwenye damu harufu ya kinywa chake na jasho lake hunuka pombe
7. Yeye hajali kutokula kama anapata pombe. Wakati mwingine ndugu hulazimika kumnywesha uji kama mtoto anapokuwa amelewa bila kula
8. Pamoja na kujaliwa uwezo mkubwa wa akili, kipawa hicho hakimnufaishi yeye, familia au hata jamii
9. Wakati mwingine hufakamia pilipili mbichi au huziponda na kunywa kama juisi akidai zinamsadia kiafya, lakini sidhani kama madai yake yana ukweli, yote hayo yanachangiwa na uraibu wa pombe. Nahisi pilipili inaweza ikawa na "kaulevi" Fulani, labda!
10. Uraibu wake wa pombe unahatarisha hata usalama wa vitu vya ndani. Akikosa hela ya pombe huviuza. Anauza mpaka vikombe vya chai
11. Kijana aliyekuwa very smart hazingatii tena usafi wake binafsi, mpaka watu wengine wanadai kuwa labda kalogwa kutokana na kuwa na akili sana
12. Uraibu wa pombe umemfanya apoteze heshima katika jamii yake iliyokuwa ikimheshimu sana.
Ingelikuwa ni ndugu yako ungefanyaje?