KWELI Inawezekana kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye VVU/UKIMWI bila kinga na usipate Maambukizi hayo

KWELI Inawezekana kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye VVU/UKIMWI bila kinga na usipate Maambukizi hayo

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU.

Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu.

08289B1B-AC79-4F6C-975E-77283B90B7FC.jpeg

Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
 
Tunachokijua
HIV ama Human Immunodeficiency Virus ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa kinga mwili, ambacho baada kuishi mwilini kwa kipindi fulani kinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI).

Virusi hawa wenye sifa ya RNA, hubeba aina 15 za protini pia huzungukwa na kuta mbili za mafuta. Hushambulia seli hai zenye vipokeo vya CD4 pekee, hubadilika mara kwa mara pamoja na kupoteza sifa ya kuishi kikiwa kwenye mazingira yasiyo rafiki.

Ili virusi viweze kuingia mwilini na kusababisha madhara huhitaji mambo matatu ya msingi-
  1. Damu au Majimaji ya mwili
  2. Kitendo hatarishi
  3. Upatikanaji wa moja kwa moja wa mishipa ya damu
Takwimu
Kwa kutumia rejea ya CDC, huu ndiyo wastani wa watu wanaopata maambukizi ya VVU/UKIMWI katika kila kundi la watu 10,000 wanaokuwa kwenye mazingira hatarishi kwa mara ya kwanza.
  • Watu 9250 kwa kupokea damu
  • Watu 63 kwa kushirikiana vitu vyenye ncha kali
  • Watu 138 kwa kushiriki tendo la ndoa kinyume cha maumbile
  • Watu 8 kwa kushiriki tendo la ndoa kwa njia ya kawaida
Kwa kuzingatia takwimu hizi za CDC, JamiiForums inatambua kuwa sio kila anayeshiriki tendo la ndoa na mtu mwenye VVU/UKIMWI pamoja na kujiingiza kwenye mazingira hatarishi kwa mara ya kwanza huambukizwa ugonjwa huu. Hata hivyo, takwimu hizi huongezeka ukubwa wake kadri mtu anavyokuwa anarudia kujiingiza mara kwa mara kwenye mazingira husika.

Uwepo wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hatua ya maambukizi ya VVU/UKIMWI, idadi ya nakala za virusi (Viral load) pamoja na udhaifu wa kinga ya mwili ya mhusika huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Kondomu kama kinga
Kwa mujibu wa USAID, Matumizi ya kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa zaidi ya 90%. Ni muhimu kutumia njia hii ili kujilinda dhidi ya gonjwa hili hatari ambalo kwa mwaka 2021 pekee liliondoa uhai wa takriban watu 650,000 duniani.

Kwa kuwa ni ngumu kujua hali ya afya ya mtu kwa kumtazama hasa kwa kuzingatia idadi ya nakala za VVU pamoja na hatua ya ugonjwa kwa wahusika, pia ili kufuta kabisa nafasi ya kuugua ugonjwa huu, ni muhimu kujilinda kikamilifu pamoja na kuepuka mazingira yote hatarishi yanayoweza kufanya uambukizwe.

Aidha, ili kupunguza nafasi ya kuambukiza wengine, waathirika wa VVU wanapaswa kutumia dawa za kufubaza makali ya maambukizi ili kudhibiti utengenezwaji wa nakala mpya za virusi, pamoja na kuongezeka kwa ukubwa wa maambukizi. Wanaofikia kiwango cha chini kabisa cha nakala za VVU hukosa sifa ya kuambukiza wengine.

Usijaribu kushiriki ngono zembe kwa imani kuwa nafasi ya kuambukizwa VVU/UKIMWI ni ndogo. Tendo la mara moja linaweza kukufanya ukanasa kwenye mtego huo.
Ikiwa mwathirika anatumia dawa ipasavyo na ukashiriki nae tendo na mpaka mkapata michubuko,je matokeo yake yatakuaje?
Je kwann asikuambukize wakat mmechubuana?
Je toka virusi kuingia mwilini vitatumia mda gan kuanza kuonekana kwenye vipimo
Kuna uwezekano visionekane hasa kwa kutegemeana na kinga ya mwili wako na zaidi pale unapokuwa kundi O la damu. Ili kuepuka mashaka na hofu zote tafadhali tumia kinga.
 
Kuna uwezekano visionekane hasa kwa kutegemeana na kinga ya mwili wako na zaidi pale unapokuwa kundi O la damu. Ili kuepuka mashaka na hofu zote tafadhali tumia kinga.
Lakini katika vipimo huchukua wastani wa mda gani virusi kuanza kuonekana
 
Huo ugonjwa unamkanganyiko mwingi sana kuna jamaa yangu kazika madem watatu kwa ngoma na yuko safi na aliishi nao kama wake zake kila akipima majibu ni yuko vizuri
Ukiwa Mzee wa tako 3 goli,

Ukimwi utausikia radioni.
 
Franco aliimba nyimbo moja hit song called "sida" kwa wadau wa lingala, chukua tahadhari kuhusu ukimwi kwani upo na baadae yeye binafsi inasemwa aliugua na kufariki. So take care guys!
 
Mi nauliza mfano, mwenza kasex Leo na mwathirika, baada ya siku tatu ukala mzigo, je utakua umeambukizwa tayari endapo mtachubuana, maana yake nahitaji shule hapa kuwa virusi huchukua muda gani mpaka kuanza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine
 
Mkanganyiko ni mkubwa sana lakini kama anatumia dawa kwa ufasaha na hana vidonda anaweza asipate maambukizi lakini haikupi uhakika, uhakika ni kucheza salama
 
Ingekuwa ukimla tu mwenye nao na wewe unao, hee nchi hii ingekuwa majumba matupu - unajichagulia tu pa kuishi.
 
Kweli
Hii inawezekana kabisa: kuna watu wako kwenye ndoa mmoja anao mmoja hana wanaitwa discordant couple.

Hii inawezekana kabisa ila jitahidi kumuandaa mwenzio ili maji ya uke yatoke ukishindwa tumia kilainishi ila pia kuna wadada maumbile yao ni makubwa kwa hivo mjamaa anateleza tu no friction.

Japo usichukulie poa tumia kondom ili uwe salama zaidi. Pia ningekupa ushuhuda ila tuache km unaweza nichek private ntakupa.
Kabisa
 
MADAI
Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU.

Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu.

Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
inashawishi tigo kwa tigo ila hapana aisee, mfuko wa malboro kuvaliwa ni muhimu.
 
Ugonjwa wa kutengeneza huu. Ila mimi mbona situmiagi kondom.. kondom inabeba dumu zima sa uume wako tunapigwa sana. Kondomu yenyew iko na madhara
 
Hii inawezekana kabisa: kuna watu wako kwenye ndoa mmoja anao mmoja hana wanaitwa discordant couple.

Hii inawezekana kabisa ila jitahidi kumuandaa mwenzio ili maji ya uke yatoke ukishindwa tumia kilainishi ila pia kuna wadada maumbile yao ni makubwa kwa hivo mjamaa anateleza tu no friction.

Japo usichukulie poa tumia kondom ili uwe salama zaidi. Pia ningekupa ushuhuda ila tuache km unaweza nichek private ntakupa.
Nipe ushuhuda
 
Back
Top Bottom