1.Cheza maeneo ya karibu na ofisi hasa zile za mizigo.,wanaposhusha mizigo huwa kunakuibeba kupanga ofisini.
Pia Kaa nao vizuri,,huwa kuna kubeba kupeleka kwa wateja
(Hapa cheza na zile ofisi zilizo maghorofani sanasana)
2.Zunguka kukusanya takataka maofisini kwa bei nafuu.
Kariakoo huwa hakuna sehemu za kutupa taka hivyo zikijaa namna ya kutupa huwa ni changamoto.
Hakikisha unapita mara kwa mara maofisini...punguza bei ya huduma ili upate wateja
3.Mchana unaweza kujumuika na wale vijana wanauza nguo za mtumba,Hasa vijora...wanaimba sana na kupiga makofi,huku wamama wakichagua.
*Hizi ntakazoweka ni nzuri ila sidhani kama zitakufaa kwa sababu bado huna pesa;
4.Asubuhi zungusha mayai ya kuchemsha
Target yako iwe kwenye maofisi...watu wananunua wananywea chai.
Hapa unaweza kujiongeza kuweka vitafunwa vingine.
5.Ungekuwa na vitendea kazi,Kuna mtu huwa anazunguka kupima presha watu maofisini.
5.Ipo biashara ya maji,ila inahitaji uvumilivu..Zungusha maji ya kunywa ofisini.
6.Biashara ya kuuza chakula.
7.Ingia Karume mtumbani,chagua nguo nzurii jeans na nightdress ,yaani zile nguo light za kuvaa wadada Hasa muda wa joto.
Komaa zungusha,target wateja kulingana na nguo ulizonazo.
Pitisha maofisini.
Sent using
Jamii Forums mobile app