Inawezekana niamkie Kariakoo na kupata kipato ikiwa sina ofisi wala chochote?

Inawezekana niamkie Kariakoo na kupata kipato ikiwa sina ofisi wala chochote?

nali rephrase , shida ni hawa mawinga chini huku (wengi wao), najua wako kwenye hustle za kutafuta mkate lakini tamaa si nzuri
wanaangalia muonekano wa mtu, au uharaka ulionao, kisha wanakupiga

majuzi natimba mtaa wa likoma pale, nafata simu ambayo najua bei yake elekezi ni 180k
nafika jamaa kaniangalia mpaka chini, kisha akanambia bei ni 260k, huu ni wizi,
nikaondoka akaniita akambia una bei gani, nikaondoka
sasa kama siyo tamaa(wizi) ni nini ?

majuzi jamaa kaleta uzi humu analalamika kapigwa fridge guard ya 15k kwa 50k
Hao sio mawinga ni matapeli tu, huu uzembe unafanywa na wenye office unakuta yy yupo dukani afu anaruhusu mtu mwngn anakua katikati ya mteja na yeye....kitu cha kawaida kinawekewa bei kubwa na wenye office wanaona powa tu!

Kingine wabongo hatutaki kujiongeza tu hivi kulikuwa na haja gani ya kumtumia winga kwenye kununua kitu kama fridge guard🤔🤔 mwingine unakuta anaulizia bidhaa flan duka hili mwenye duka kama hana anakwambia twende sehem flan na kwel unaenda 🤔
 
Hao sio mawinga ni matapeli tu, huu uzembe unafanywa na wenye office unakuta yy yupo dukani afu anaruhusu mtu mwngn anakua katikati ya mteja na yeye....kitu cha kawaida kinawekewa bei kubwa na wenye office wanaona powa tu!

Kingine wabongo hatutaki kujiongeza tu hivi kulikuwa na haja gani ya kumtumia winga kwenye kununua kitu kama fridge guard🤔🤔 mwingine unakuta anaulizia bidhaa flan duka hili mwenye duka kama hana anakwambia twende sehem flan na kwel unaenda 🤔
Usimamizi Tu sio mzuri..mawinga wanaweza dhibitiwa kabisa na wakapewa vitambulisho
 
Wakinga na Wachaga au watanzania wanaoagiza mzigo kutoka China mara nyingi huuza wenyewe mizigo yao tofauti na wachina. Wachina huagiza mizigo kwao kwa simu tu, ambao naamini bei zao za manunuzi huko kwao zina punguzo maalum (kwa maana raia wa nchi mzigo utakapo) hivyo kufanya mzigo wanayo agiza wao kuwa cheap.

Kwa kujibu swali lako, ni hivi, wao wachina mfano kwa case ya viatu ama yeboyebo na bidhaa nyingine, hufungua mzigo wa aina mpya karibu kila siku.

Yale maduka uyaonayo wanaweka tu display lakn mzgo hasa huwa store eneo lingine. Sasa katika zile aina tofuati, huwa kunatokea ambayo hupendwa na wateja kupitiliza. Kwahiyo wewe dalali kwa hela yako, unaenda kwa huyo muuzaji unaununua huo mzigo wote kisha unauuza wewe kwa kuongeza bei kidgo juu yake. Lakn hapa lazma uwe na mtaji na ujulikane na ulijue soko vizuri.

Ukishakuwa tajir na una hela ya kutosha, basi ukisikia mfano (usininukuu lakan) kipodizi fulani original kinatembea sokoni wewe unapanda fasta china kwenda kuleta feki yake. Ukisikia piituuu zinakimbia wanaenda kuleta feki yake nk. Kwahiyo lazma uwe na mtaji na lazma uwe na uzoefu kdgo wa kuwa maeneo husika na kukutana na watu husika.

Ushauri wangu kwa Serikali mara zote ni mmoja tu, wasiruhusu importers hasa wakigeni kuwa retailers at same time. Hakuna sehm duniani wanaruhusu hilo. Yaani mchina anapoagiza mzigo kwao anakuwa na punguzo la bei, yy hasafiri zaidi ya kuagiza. Akifika hapa anashindana na raia ambaye ana container chache anayenunua bei juu huko china, ana mkopo wa riba kubwa kodi nyingi wanashindania soko moja.

Duniani kote ujasusi wa uchumi ni kulinda mapato ya nchi na kuwalinda ama kuwapa upendeleo raia wako kwny soko la nchi yako dhidi ya mgeni, ikiwepo Ajira.

Kwa kufanya hivyo Serikali inatakiwa iwe na sheria moja kali sana, wachina na raia wa nje wanapo import mizigo kwa bulk kutoka nje, wasiruhusiwe kuuza rejareja wakishindana na mmachinga. Chukulia muhindi aagize mitumba halafu baada ya kuagiza na yy auze rejareja karume ilala tandika nk.

Muhindi akifanya hivyo lazma ataua kazi za wamachinga. Kwahiyo endapo Serikali ingewatengea importers eneo lao na kupiga marufuku importers kuwa wauzaji rejareja, kwa swali lako inamaana mtu yoyote kwa mtaji wowote anachagua niche yake, anaenda kununua kwa wachina kisha anauza rejareja, hapa Serikali inakuwa imetengeza Ajira na kodi mpya na imelinda raia wake.

Hivi Mtanzania anaruhusiwa kwenda china halafu aagize mzgo kutoka Tanzania na kisha akiwa kule auuze rejareja? Ataambiwa umeshaleta china sharti uuze kwa mchina, baada ya hapo tembea. raia wao watauza wenyewe rejareja kwa bei zao.
Watu wasiofahamu tu ndio wanaofikiri kuwa hawa wachina wanategemea hizi biashara. Hao watu wapo wengi kwenye haya mataifa masikini kwa ajili ya kufanya international money laundering wakishirikiana na drug cartels/kingpins. Hakuna watakatishaji wakubwa wa pesa duniani kama wachina. Waulize USA jinsi wanavyohangaika nao . Mabilioni ya pesa yanatakatishwa daily huku watu wakidhani kuwa hao watu wapo huku kwa ajili ya hizi biashara za kudunduiza. Wachina walishavuka huko na kwenye soko huwezi kushindana nao maana wao faida zao hawategemei ktk kuuza hiyo mizigo ya kutoka china.
 
Inakuwaje mtu unatumia winga na upo Dar? Huwa sielewi..sema wengi wetu ni uvivu tu...na ukishakuwa mvivu hata biashara itakupa tabu. Uzuri wa kariako Maduka mengi ya bidhaa za aina moja yako eneo moja...katika hayo maduka kuna chimbo la hiyo biashara LAZIMA...umeshinda vip kulitafuta? Sign kubwa ni ukiwahi sana asubuhi duka lilojaza vijana wengi wananunua hilo ni chimbo mojawapo.
 
Watu wasiofahamu tu ndio wanaofikiri kuwa hawa wachina wanategemea hizi biashara. Hao watu wapo wengi kwenye haya mataifa masikini kwa ajili ya kufanya international money laundering wakishirikiana na drug cartels/kingpins. Hakuna watakatishaji wakubwa wa pesa duniani kama wachina. Waulize USA jinsi wanavyohangaika nao . Mabilioni ya pesa yanatakatishwa daily huku watu wakidhani kuwa hao watu wapo huku kwa ajili ya hizi biashara za kudunduiza. Wachina walishavuka huko na kwenye soko huwezi kushindana nao maana wao faida zao hawategemei ktk kuuza hiyo mizigo ya kutoka china.
😂😂😂😂😂dah ila Tz raha sana
 
Nimeishia kisoma hii paragraph, asee itoshe kusema tu ubinadamu kazi sana. Mtu yupo radhi kuangamiza raia wenzake kisa tu ajitajirishe.

Aaahh ni balaaa sana. Kuanzia dawa, vinywaji, vyakula yani kila bidhaa ni fake (haifai kwa matumizi ya binadamu) ila ndio hivyo sasa tunajaziwa sokoni.
Hivi ndivyo waafrika tulivyoupokea ubepari mkuu, ili kufanikiwa lazima udhuru au uumize wengine, ujamaa ulishatushinda na ubepari hatuuwezi sijui tukae wapi
 
Hivi ndivyo waafrika tulivyoupokea ubepari mkuu, ili kufanikiwa lazima udhuru au uumize wengine, ujamaa ulishatushinda na ubepari hatuuwezi sijui tukae wapi
Tuko katika hali mbaya sana. Turudi kwenye kuamini mambo ya kiasili zaidi, bora kutumia bidhaa za asili zaidi kuliko hizi za wazungu maana kila uchwao watu wanafanya genetic engineering ku clone watu jinsi watakavyo.

Kwa sehemu kubwa ni hawa giant tech and pharma companies wanataka kujitajirisha zaidi kwa kutengeneza shida ambazo wao wenyewe through back doors watakufata kukuambia wanaweza kukusaidia kuzi solve.

Imagine cancer wameshindwa kuitibu wanakupa relief through chemo which is worse.

Tumeishaa Jadda.
 
Inawezekana niamke asubuhi na kwenda Kariakoo ikiwa Sina ofisi yeyote hapo???? Udalali huwa unafanywaje jamani!

Kazi gani unaweza kuifanya pale Kariakoo kwaajili ya kukuingizia chochote kitu ikiwa huna duka, huna chochote?
Kuna unaemfahamu anadili kitu chochote? winga karikaoo kwa siku hukosi 20 elfu! ata kama ni fundi simu ila unatumwa tu kwenda dukani kununua space na mafundi wenyewe unapata hela fresh tu
 
Mhmhm! Kipato bila ofisi wala kazi yoyote???
Hii imeekaake doh!
Ngoja nisome vizuri kwanza
 
Mimi nakushauri tu nenda mwenyewe uwanja wa vita ukajifunze na kujionea. Jipe muda usitake kuwa kama uliowakuta kwenye mishe mishe utakayoona utaiweza

Mimi naamini kwa kujifunza na kujionea utapata muongozo mzuri sana.

Kama kiingereza kinapanda soma soma na hivi vitabu ili kujifunza (na ujifunze kweli sio ilimradi usome maana wafu wengi wanasoma ila hawajifunzi)

1. 48 laws by Robert Green
2. 50th Law by 50 Cent
3. Time to Boss up by Rick Ross
4. The Prince by Nicolo Machievelle
5. Book of 5 Rings by Miyamoto Musashi
5. Hustle harder hustle smart by 50 Cent
6. Biblia na Quran (bila kujali imani yako)

Mkuu kila la heri, ila usome kujifunza hapo inabidi nisisitize maana wengi wanasoma ili kusoma tu, kujifunza inaitaji uwe makini.
 
Mda mwingine laana ni mtazamo!

Kariakoo mchina analeta mzigo kutoka viwandani kwao Labda mkuranga, jpili anatuma Kazi kwenye magroup wanatokea watu baada ya kupima upepo wakagundua Kazi inatembea sana watu wameweka order wengi yy anamlipia mzigo wote Labda 45M.

Mwanzon mzigo ulikua unasoma hv

DB8529-6
36-41
PC 48
5500


Baada ya tajir kulipia wote inasoma hv

DB8529-6
36-41
PC 48
6500

Hao wote ni mawinga ktk level tofauti ya mitaji! Hapo laana ipo wapi?
Kama uko Kwa magroup hayo naomba msaada WA kujiunga
 
Kuna msemo wa kizaramo nimeusikia Jana,nimesahau kilugha Ila tafsiri yake inasema "ukitaka kutunzwa,ingia kati ucheze"....vijana tunapenda sana kuulizia ulizia Mambo tukiwa mbali,panda gari nenda kariakoo ukajionee au ukaulizie watu ambao tayari wapo pale
 
Back
Top Bottom