karonga
JF-Expert Member
- Mar 19, 2017
- 681
- 1,128
Wewe jamaa lengo lako ni zuri lakini hichi kiswahili chako ulichoandika nina uhakika wewe ni mchina 100% bora tu utuache tusiyafanye makubwa[emoji16][emoji16][emoji16]Wakinga na Wachaga au watanzania wanaoagiza mzigo kutoka China mara nyingi huuza wenyewe mizigo yao tofauti na wachina. Wachina huagiza mizigo kwao kwa simu tu, ambao naamini bei zao za manunuzi huko kwao zina punguzo maalum (kwa maana raia wa nchi mzigo utakapo) hivyo kufanya mzigo wanayo agiza wao kuwa cheap.
Kwa kujibu swali lako, ni hivi, wao wachina mfano kwa case ya viatu ama yeboyebo na bidhaa nyingine, hufungua mzigo wa aina mpya karibu kila siku.
Yale maduka uyaonayo wanaweka tu display lakn mzgo hasa huwa store eneo lingine. Sasa katika zile aina tofuati, huwa kunatokea ambayo hupendwa na wateja kupitiliza. Kwahiyo wewe dalali kwa hela yako, unaenda kwa huyo muuzaji unaununua huo mzigo wote kisha unauuza wewe kwa kuongeza bei kidgo juu yake. Lakn hapa lazma uwe na mtaji na ujulikane na ulijue soko vizuri.
Ukishakuwa tajir na una hela ya kutosha, basi ukisikia mfano (usininukuu lakan) kipodizi fulani original kinatembea sokoni wewe unatembea sana sokoni wewe unapanda fasta china kwenda kuleta feki yake. Ukisikia piituuu zinakimbia wanaenda kuleta feki yake nk. Kwahiyo lazma uwe na mtaji na lazma uwe na uzoefu kdgo wa kuwa maeneo husika na kukutana na watu husika.
Ushauri wangu kwa Serikali mara zote ni mmoja tu, wasiruhusu importers hasa wakigeni kuwa retailers at same time. Hakuna sehm duniani wanaruhusu hilo. Yaani mchina anapoagiza mzigo kwao anakuwa na punguzo la bei, yy hasafiri zaidi ya kuagiza. Akifika hapa anashindana na raia ambaye ana container chache anayenunua bei juu huko china, ana mkopo wa riba kubwa kodi nyingi wanashindania soko moja.
Duniani kote ujasusi wa uchumi ni kulinda mapato ya nchi na kuwalinda ama kuwapa upendeleo raia wako kwny soko la nchi yako dhidi ya mgeni, ikiwepo Ajira.
Kwa kufanya hivyo Serikali inatakiwa iwe na sheria moja kali sana, wachina na raia wa nje wanapo import mizigo kwa bulk kutoka nje, wasiruhusiwe kuuza rejareja wakishindana na mmachinga. Chukulia muhindi aagize mitumba halafu baada ya kuagiza na yy auze rejareja karume ilala tandika nk.
Muhindi akifanya hivyo lazma ataua kazi za wamachinga. Kwahiyo endapo Serikali ingewatengea importers eneo lao na kupiga marufuku importers kuwa wauzaji rejareja, kwa swali lako inamaana mtu yoyote kwa mtaji wowote anachagua niche yake, anaenda kununua kwa wachina kisha anauza rejareja, hapa Serikali inakuwa imetengeza Ajira na kodi mpya na imelinda raia wake.
Mtanzania anaruhusiwa kwenda china halafu aagize mzgo kutoka Tanzania na kisha akiwa kule auuze rejareja? Ataambiwa imeshaleta china uuze kwa mchina, baada ya hapo tembea raia wao watauza wenyewe rejareja kwa bei zao.