Inawezekana niamkie Kariakoo na kupata kipato ikiwa sina ofisi wala chochote?

Wewe jamaa lengo lako ni zuri lakini hichi kiswahili chako ulichoandika nina uhakika wewe ni mchina 100% bora tu utuache tusiyafanye makubwa[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mi ndio nampenda sasa, nyinyi ndugu zangu katika Imaan mmefeli!
Rose Ndauka angekuwa anasubiria wa imani yake, si ajabu angekuwa anapuyanga hadi leo.

Ona sasahivi Rose,ametulia,amenawiri yaani maisha yake yanamuendea vizuri.
Mungu alimuandikia huko.


Na wewe usisite,wasije wakakutisha,
Wewe kama moyo wako umepata amani na rizki yako ipo huku,,karibu Kanisani wifi,huku ukiendelea kuyafurahia maisha.

Mungu ni yuleyule.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa zipo mingi we nenda katafute changamoto alafu zitatue kama msosi wanauza ghali tafuta namna wapate kwa bei rahis, kusapply, etc n mambo mengi
 
Maneno mengi wakati mtu kasema Hana pesa
 
Ndizi mzuzu.

Zile zinazokuwa Tamu Zina sukari.

Moro na Tanga ziko
 
Ungeomba namba ya mpesa ya mtoa mada umtumie walau elf 5 ya kula, akafanye kazi, ningekuona wa maana Nifah
 
Si ufike huko kkoo kwanza ukafanye tathimini?unaulizia mchongo umekaa geto kwenye kasofa ka one sitter unaperuz🤣🤣
Ukitaka uhondo wa ngoma,ingia ucheze👌
 
Nimeishia kisoma hii paragraph, asee itoshe kusema tu ubinadamu kazi sana. Mtu yupo radhi kuangamiza raia wenzake kisa tu ajitajirishe.

Aaahh ni balaaa sana. Kuanzia dawa, vinywaji, vyakula yani kila bidhaa ni fake (haifai kwa matumizi ya binadamu) ila ndio hivyo sasa tunajaziwa sokoni.
 
Kwel watu wengi kabla hamjajipata kumbe mlipita kkoo
 
acha na uwinga, ni kazi ya wizi na ulanguzi yenye laana
Mda mwingine laana ni mtazamo!

Kariakoo mchina analeta mzigo kutoka viwandani kwao Labda mkuranga, jpili anatuma Kazi kwenye magroup wanatokea watu baada ya kupima upepo wakagundua Kazi inatembea sana watu wameweka order wengi yy anamlipia mzigo wote Labda 45M.

Mwanzon mzigo ulikua unasoma hv

DB8529-6
36-41
PC 48
5500


Baada ya tajir kulipia wote inasoma hv

DB8529-6
36-41
PC 48
6500

Hao wote ni mawinga ktk level tofauti ya mitaji! Hapo laana ipo wapi?
 
nali rephrase , shida ni hawa mawinga chini huku (wengi wao), najua wako kwenye hustle za kutafuta mkate lakini tamaa si nzuri
wanaangalia muonekano wa mtu, au uharaka ulionao, kisha wanakupiga

majuzi natimba mtaa wa likoma pale, nafata simu ambayo najua bei yake elekezi ni 180k
nafika jamaa kaniangalia mpaka chini, kisha akanambia bei ni 260k, huu ni wizi,
nikaondoka akaniita akambia una bei gani, nikaondoka
sasa kama siyo tamaa(wizi) ni nini ?

majuzi jamaa kaleta uzi humu analalamika kapigwa fridge guard ya 15k kwa 50k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…