Inawezekana shauku ya kufanya tofauti na mtangulizi wake ndiyo inayomponza?

Inawezekana shauku ya kufanya tofauti na mtangulizi wake ndiyo inayomponza?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Ni swali ambalo linaweza kuwa na majibu ya ndio na sio kutokana na hali halisi.

Alipoingia tu madarakani 'kwa kudra' kama alivyojinasibu, alifanya mabbadiliko mengi kwa haraka na pengine kwa kutaka kuridhisha kundi dogo la watu wenye maisha bora maarufu kama wawekezaji.

Huku watanzania wa hali ya chini wakitwishwa mzigo wa kodi na tozo na kuwapa nafuu hao 'wawekezaji'

Je, hayo na mengine mengi yaweza kuwa chanzo cha kuyumba zaidi kwa uchumi na kuongezeka kwa gharama za maisha hasa kwa wananchi wa hali ya chini?
 
"... Mama muweke huyu, na huyu pia baba yake ametusaidia Sana, pia yule apewe angalau ka ukuu wa Mkoa maana ana kundi kubwa ambalo ni tegemeo kukuvusha 2025... "

Wakati wapo kwenye huo ujinga miradi ya kimkakati yote imesimama, dawa hospitali hakuna, ....na siku si nyingi Bakhresa atakopwa ili kulipa mishahara ya watumishi.
 
Ukitazama hii clip ndio utajua akili za washauri zikoje.

Watu wanawaabudu ngozi nyeupe sidhani kama Taifa tuna msaada wowote.

".... Mama muweke huyu, na huyu pia baba yake ametusaidia Sana, pia yule apewe angalau ka ukuu wa Mkoa maana ana kundi kubwa ambalo ni tegemeo kukuvusha 2025.... "
Wakati wapo kwenye huo ujinga miradi ya kimkakati yote imesimama, dawa hospitali hakuna, ....na siku si nyingi Bakhresa atakopwa ili kulipa mishahara ya watumishi.

Ukitazama hii clip ndio utajua akili za washauri zikoje...
Tupambanie KATIBA mpya ndugu zangu Watanzania,

Tupate viongozi wenye MAONO watakaoendana na MAONO yatokanayo na Katiba tutayoandika.

Binti mmoja wa mfalme alipocheza vizuri mbele ya babaye mfalme, aliambiwa omba chochote nitakupa,

Kwakuwa Yeye hakuwa MAONO yoyote, alikimbilia Kwa mamaye akamuuliza niombe nini, mamaye kamjibu, niletee KICHWA Cha yule JOHNBAPTIST kwenye sinia na akaletewa, sijui alipata faida Gani!!!!!
 
".... Mama muweke huyu, na huyu pia baba yake ametusaidia Sana, pia yule apewe angalau ka ukuu wa Mkoa maana ana kundi kubwa ambalo ni tegemeo kukuvusha 2025.... "
Wakati wapo kwenye huo ujinga miradi ya kimkakati yote imesimama, dawa hospitali hakuna, ....na siku si nyingi Bakhresa atakopwa ili kulipa mishahara ya watumishi....!
😃 Sio kwamba watamkatia kipande cha ardhi na kisha kuwataka wananchi wa eneo husika wapishe muwekezaji?
Walahi ile sauti naisikia kwa mbaali "kuna siku nchi itapigwa mnada hii"
 
Back
Top Bottom