Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 6,479
- 4,974
Idara zote za serikali nina maana serikali nzima zina mlipaji mkuu mmoja ambaye ndiye katibu mkuu wa hazina.Najua humu Kuna wajuzi wengi sana waliohudumu na wanaohudumu serikalini na maeneo mengine, in fact, wakurugenzi pia wapo humu hivyo Nina Imani hoja yangu itapata mashiko na msaada wa kutosha.
Inashangaza kuikuta shule Haina photocopy machine Wala printer. Haina meza nzuri Wala viti. Swali langu ni, je, inaruhusiwa na inawezekana shule ya serikali kukopa benki?!!!!!!! Utaratibu upoje?!!
Karibuni kwa elimu kutoka kwa waungwana, matusi kutoka kwa wehu na kashfa kutoka kwa waliovurugwa.
πππ
Ahsante sana kwa elimu nzuri.Kiongozi, Pole sana kwa changamoto uliyokutana nayo
Ili mtu akidhi vigezo vya kukopa bank ni lazima azalishe/awe na kipato cha kuaminika au awe na dhamana ya kueleweka. Ninavyojua shule za Sekondari za Serikali zilizo nyingi hazizalishi/hazina vipato vya uhakika lakini pia huwezi kutumia chochote kuiwekea dhamana kwani sio mali yako. Kwa maana hiyo, itakuwa imekosa vigezo vya kukopesheka.
1. Kama shule inauhakika watapata hela ya kulipa deni, basi waitumie hiyo hiyo kununua kimoja kimoja
2. Mkuu wa shule awasiliane na bodi ya shule kuona kama itamruhusu achangishe wazazi walau kidogo kidogo (ya ukarabati kila mwaka) japo hii inategemea na mkoa ilipo.
3. Mkuu wa shule awe ana andaa harambee wakati wa mahafali ya mwaka na kutaja kabisa anachotaka kufanya. Huwezi jua kama kuna wazazi wenye uwezo wakiguswa watamsaidia.
Wazo la kuchangisha wazazi,wadau,vyama vya ushirika nk ni wazo zuri sana! Tuko tayari kuchangia Harusi kila mwaka na Maendeleo ya shule wa Tanzania tuko tayari kuchangia wakati wowote.Wasiliana na viongozi wako Maafisa Elimu wakisaidie viti , printer na photocopy mashine ongea na wazazi wachangie.