Inawezekana Tanzania haijawa Tayari kwa mashindano makubwa ya kimataifa yanayoihusu timu ya Taifa

Inawezekana Tanzania haijawa Tayari kwa mashindano makubwa ya kimataifa yanayoihusu timu ya Taifa

Kenya wametoka kifungoni si muda mrefu, lazima watakuwa na mzuka tofauti na sisi ambao mashindano ya kimataifa yamekuwa mengi na yanafanyika kila siku nchini.

Pia uchumi wetu ni mdogo, hatutaki kukubali na tupo out of touch kwa kutofahamu hilo. Hiyo 2,000/= mnayoona ni ndogo sana ni kubwa kwa waendaji viwanjani ukijumuisha na nauli.

Lakini kubwa zaidi ambalo hatutaki kukubali ni hali ya kisiasa nchini na michezo kuingizwa kinyemela au waziwazi katika siasa. Kwa kuwa watu hawana jinsi ya kuonyesha kupinga hayo wanaamua kususa.
Na katika nchi za east Africa tumezidiwa na warundi Tu kwa umaskini wa mtu mmoja mmoja
 
Timu ya Taifa ni timu yetu ya KISERIKALI dhalimu ya Fisiemu….. watu wanavinyongo na serikali mkuu
Na mbaya zaidi ni pale CCM inapoingiza siasa kwenye mpira kwa kutumia fursa hiyo kumnadi Mgombea wa Fisiemu
 
Kenya wametoka kifungoni si muda mrefu, lazima watakuwa na mzuka tofauti na sisi ambao mashindano ya kimataifa yamekuwa mengi na yanafanyika kila siku nchini.

Pia uchumi wetu ni mdogo, hatutaki kukubali na tupo out of touch kwa kutofahamu hilo. Hiyo 2,000/= mnayoona ni ndogo sana ni kubwa kwa waendaji viwanjani ukijumuisha na nauli.

Lakini kubwa zaidi ambalo hatutaki kukubali ni hali ya kisiasa nchini na michezo kuingizwa kinyemela au waziwazi katika siasa. Kwa kuwa watu hawana jinsi ya kuonyesha kupinga hayo wanaamua kususa.
Mbona timu pendwa watu wanaenda kwa wingi viwanjani tena viingilio kuanzia VVIP 1M hadi regular 5,000?

Tatizo sio uchumi mdogo….. tatizo hilo umelotaja hapo mwishoni
ni UZALENDO Fisiemu wametuondolea, kila kitu cha serikali watu wanakua na vinyongo
 
Hata hizo timu pendwa tungekuwa zinacheza kila baada ya siku tatu sehemu moja ungeona matokeo
 
Tatizo ni kipindi cha siasa za uchaguzi huku zikiwa na zenyewe hazina afya.

Wananchi ni kama wanapambana na hali zao.
 
Nimejaribu kufuatilia mwenendo wa mashindano haya ya CHAN hasa ushiriki wa mashabiki uwanjani, ukweli ni kuwa Tanzania bado sana. Sio tu mashabiki, hata viongozi wenyewe ni kama vile wanajilazimisha tu kujihusisha na CHAN ila wako serious sana na siasa. Inawezekana vipi timu ya Taifa inacheza alafu uwanja ni mtupu? Katika mechi zote tatu za Stars hakuna mechi hata moja tumejaza uwanja. Tutatia aibu sana mashindano ya 2027. Kuna wakati naona bora mashindano ya 2027 yahamishwe tu. Ladha ya soka ni mashabiki, sasa watu wamefanyiwa 2000 kiingilio na hawaendi uwanjani, seriously? Picha hapo chini ni mechi ya Stars ya Jana vs MadagascarView attachment 3437199View attachment 3437200​
Unapanga mechi usiku wa saa 2 mtu unatokea Bunju, Boko, gongo la mboto na timu yenyewe taifa stars?
 
Ishu ya kwanza ni hamasa lakini pia lazima Serikali ikubali kuingia gharama kulipia mashabiki inapofika kwenye timu ya taifa. Mechi na guinea kufuzu uwanja ulijaa
 
Mimi nasubiria tu siku ya Mwananchi! 💛💚 Tena nitanunua jezi kwa gharama yoyote ile! Na pia nitalipia kiingilio! Nitasafiri kutoka Mkoani! Nitakuja mjini na kufikia kwenye lodge na wife wangu! Yaani ni full kuunguza pesa!Tutakula! Na tutashangilia pamoja na Wananchi wenzangu!

Hiyo timu ya Taifa Stars ni mali ya CCM, Karia na Samia. Hata watu wasipo jitokeza kwa wingi, ni sawa tu. Na kwa hao wanaojitokeza, ni vizuri mkawapongeza.
Yanatoka akilini kweli ndugu hayo
 
Back
Top Bottom