Inawezekana tumemezeshwa matangopori mengi sana kabla ya kuenea kwa teknolojia na kufurika kwa hizi smartphones. Christy Chung yupo hai bana!

Inawezekana tumemezeshwa matangopori mengi sana kabla ya kuenea kwa teknolojia na kufurika kwa hizi smartphones. Christy Chung yupo hai bana!

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Alaaniwe yule mtangazaji wa redio (kama siyo tbc basi ni radio free) ambaye alitangaza kwamba mdada (mmama) yule amekufa. Ili nisiwaache wengine hapa ngoja nifafanue kidogo, huyu Christy Cheung ni yule mdada aliyekuwa akilindwa na Jet Li kwenye movie ya The Bodyguard From Beijing

Kipindi hicho nikiwa sekondari nakumbuka nikiwa nyumbani hunibandui kwenye kiredio changu cha Rising nimefunga antena ndefu ya waya. Nilikuwa napenda sana vipindi fulani fulani na watangazaji fulani fulani kwenye redio fulani fulani.

Nakumbuka redio pendwa kwangu ilikuwa ni Radio Free Afrika, Radio One, TBC FM na Sauti Ya Injili. Baadaye zikaja Radio Five, Uhuru FM, Nyemo FM, Abood, Radio Imani, MUM na redio nyingine jina nimesahau ambayo ilikuwa yenyewe ni kingereza tupu na ndipo nilipomjuliaga Vanessa Mdee huko na kumpenda sana

Watangazaji ninaowakumbuka (majina tu sura sizijui) ni Rahabu Fungo/Fred, Fred Waa, Badi Sangu, Julius Nyaisanga, Dijaro Arungu, Felista Kurugila, Elia Migongo, Jumaa Baragaza, na wengine naona wananitoka bana. Lakini tuache utani RFA ilikuwa juu sana kipindi kile, kuna wadada kama watatu hivi na wajamaa watatu kwenye kusoma habari raha sana ukiwasikiliza

Vipindi asilimia kubwa na utoto niliokuwa nao nilikuwa napenda miziki tu na baadhi ya vipindi vya manufaa ya kawaida mfano search line, mambo mambo, miziki ya kihindi kama siyo Tuesday ni Thursday, bunga bongo, vipindi vya kutuma salamu kuna jamaa anaitwa Yisuf Kichogo yeye ni msikilizaji redio Abood simsahau. Radio nyingine zilikuwa bado ni mpya hivyo kuzipenda kwangu ni kwa ajili tu ya miziki maana redio ikiwa mpya ilikuwa ni mziki bandika bandua

Radio Nyemo walikuwa Ijumaa wanaleta Sheikh wa Kishia (ahlul bayt) nilikuwa sikosi kuwafuatilia mafundisho yao. Radio imaan walikuwa wana vipindi vizuri sana vya maswali ya dini na ndipo nilijifunza kuwa Nuhu alikufa akiwa na miaka zaidi ya 1000 na siyo 950 kama waislamu wengi wanavyokariri. Sauti ya Injili wao walikuwa na kipindi chao Soma Nasi kama sikosei aisee nilikuwa nakipenda sana hiki! Nitaleta uzi kuhusu hizi redio na televisheni za dini ngoja niishie hapa kwanza usije ukasahau hata nilikuwa nazungumzia nini

Turudi sasa kwenye hoja yangu, ni kwamba moja ya vipindi nilikuwa nafuatilia ni vile vipindi vya historia na matukio mbali mbali kwa mfano unaelezewa siku kama ya leo kulitokea jambo gani likaacha historia au nani maarufu alizaliwa na nani amekufa siku kama ya leo. Sasa siku hiyo mtangazaji (ni vile sikumbuki tu jina lake lakini nina uhakika hatoki nje ya redio mbili hizi RFA na TBC hasahasa TBC) akawa anaendesha kipindi na kilikuwa kina parts mbili, kinataja kwanza yale ya furaha katika kumbukumbu kisha kinamalizia yale ya huzuni.

Basi akasema "leo bwana kwa upande wa huzuni tuna msiba kwa wale wapenzi wa filamu yule dada aliyeigiza na Jet Li kwenye movie ya The Bodyguard From Beijing amefariki huko China". Nakumbuka mtangazaji akachambua kidogo kuhusu dada yule na kuhusu Jet Li mwenyewe. Basi kwa kuwa enzi hizo vijana tumeozea kwenye miziki na movies nilikuwa mnyonge sana ukizingatia movie yenyewe ilikuwa ni namba wani kwangu. Nikawa kila nikiiangalia movie ile napatwa na huzuni aisee

Sasa leo katika pitapita zangu kwenye mitaa ya Google nashangaa nakuta taarifa za kuonesha yule mwanamama yupo hai nikasema labda nimechanganya mambo nikaanza kumgoogle vizuri nakuta hakuna taarifa yoyote kuhusu kifo chake. Nikasema niihusishe akili mnemba nayo inaniambia vivyo hivyo kwamba hakuna taarifa ya kifo chake tena yenyewe imeenda mbali zaidi kwamba katika waigizaji wakuu wa ile movie hakuna hata mmoja aliyekufa. Nikasema labda nimgoogle Michelle Yeoh huenda labda nimechanganya mafaili bado hata yeye ni mzima wa afya!

Ama kweli watangazaji wa zamani mlijua kutuweza...!
 
Back
Top Bottom