Uchaguzi 2020 Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii ya T 2020 JPM?

Hahah hio namba ni specific kwa kampeni season. Inalipiwa laki na nusu na si 10M mjomba.
 
Hii ni udhibitisho wa kukosa umakini katika utendaji labda kwa sababu ya woga. Lazima mamlaka ya juu itakuwa imependezwa na hizo namba na hivyo haijalishi madhara
 
Magari ya umma yanatumika na CCM, ili kuficha yakapewa hizo number.

Nimekumbuka hadithi ya KALUMEKENGE.
 
Ni hivi, hizo ni private number na zinalipiwa TRA.
Hata wewe kama una gari 5 na zote unataka kuweka jina lako (Rrondo) ni pesa yako tu

Uzuri na ubaya wa mambo haya huwa yanaacha foot print! kesho Tundu Lissu akilianzisha msije sema ana kiherehere
 
Ni hivi, hizo ni private number na zinalipiwa TRA.
Hata wewe kama una gari 5 na zote unataka kuweka jina lako (Rrondo) ni pesa yako tu

We hujawaza kwa kina, private number ikishachukuliwa na mmoja, hiyo namba anapewaje tena mwingine? Halafu kuna watu wamekupa na LIKE aisee ushabiki bila kutumia akili ni mbaya sana.

Hata kama ni magari ya mtu mmoja, lazima iwekwe tofauti.. mfano kama mwenye hayo magari anaitwa MIMI, inaweza ikaandikwa MIMI 1, MIMI 2, MIMI 3 etc... huwezi yote ukaandikiwa MIMI, MIMI, MIMI.

Acheni kutetea vya kijinga

Fikiria, umekutana na trafiki anakagua magari kwa vile vimashine vyao, kama inadaiwa akaona T 2020 JPM inadaiwa, atamkamata nani?
 
Nawewe mpaka wakugonge ulikuwa unafanya nini? Au ndio kutafuta visa tuu?

Zimesalia siku chache kufika kwenye uchaguzi usikae kumchagua JPM.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Kwa hoja hii BAVICHA wameona itawaongezea kura.

Bozo kweli kweli
 
Mbuzi hula kulingana na urefu wa Jamba yake. Unafikiri CCM Ni wajinga hawaelewi misemo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…