Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Pain killer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
14,365
Reaction score
21,747
Habari wakuu

Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.

Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.

Nimesikitika sanaa.

Uzi tayari!
 
Kipindi hiyo ilikuwa ni kula bata tu miaka ya 2000 wakuja wengi walikuja na mafuriko ya elninyo ndo wamejenga. Aliimba Rr Remmy wote tukiwa mafundi viatu nani atamshonea mwenzie?
Wote tukimiliki nyumba nani atapanga?
We jenga wengine wapange.
Mi ndo kwanza napanda mihogo huku.
 
Watu wamezaliwa mikoani uko mwaka 1970-80s na mbka leo hawana viwanja kumbuka ni mikoani sembuse uyo wa Dar,,, jero kipindi chake ukiikamata wewe upo vizur kiuchumi maana nakumbuka babu alinambia mbka anastaafu alikua analipwa 1700 alkua mfanyakazi wa serikali uyo na alikua doni tu kijijini.
 
Back
Top Bottom