Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Dar kuna watu wangapi na hekari ngapi zinazoweza kupimwa na ili kila mtu apate kiwanja cha ukubwa gani ?

Huko tunakoelekea kiwanja / nyumba huenda isiwe asset tena (mwendo wa matozo) hivyo watu kujikita kwenye mortgages kiwanja au nyumba ni iwapo tu kinaingiza pesa na sio kutumia pesa
 
Wazee wetu walipo kuwa vijana walikuwa wavivu wa kufikiri kuhusu maisha wengi wao walikuwa Wana jua walipo tu na walikuwa hawajui Kesho Yao itakuwaje wao walikuwa wanaishi tu
 
Pesa ilikuwaa ngumu kwa kipindi hiko kama ambavyo ni ngumu kununua kiwanja mil 6 kwa Sasa hivi. Ndio ilikuwa ni aghali kununua kiwanja kwa laki 1 kipindi hiko. So usiwatukane watu.
Hapana nakukatalia kuna ndugu yetu alikuwa mwanajeshi ana jutia mpaka leo wakati yupo kijana walipewa Viwanja bure kunduchi mwenyekiti alikuwa ana wafata kazin ana waambia waje awagaiye Viwanja ili wajenge nyumba karibu na kazini kwao kuliko kutoka mbali lugalo kwenda kufanya kazi kunduchi wakatio kunduchi ni mapoli alivyo kuwa ana waambia walikuwa Wana kataa Wana sema hawa wezi kukuaa mapolini wakati kiwanja Wana gaiwa bureee
 
Aiseee ila ana nyumba tayali
NYUMBA sio BIG ISSUE kwa MBUNGE WA VITI MAALUM aliyehudumu kwa kipindi cha miaka kumi [ 10 ] BUNGENI.

BIG ISSUE ni kuwa BANK TELLER!! Ina maana hana fursa nyingine mpaka akafanye kazi ya UKARANI WA BENKI? Ameshindwa hata kuwa MENEJA WA TAWI LA BENKI?

Hizo kazi za UKARANI WA BENKI ni AJIRA zetu sisi kama VIJANA, sasa kuvamiwa na WAHESHIMIWA inakuwa haileti PICHA nzuri 😁😁

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa alikuwa ni MTU WA DAGI na ANASA sana, ndio maana CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM βš’οΈ walimtema.
 
na weww mwanao atakujaa na uzi kama hii
 
Yupi huyo.?
Kuna MAKALA moja iliandaliwa na kituo cha televisheni cha SAFARI CHANNEL na kurushwa hewani na TBC1.

Ilikuwa inahusu familia ya SPIKA MSTAAFU, ADAM SAPI MKWAWA! Kwa kweli ile sio PICHA nzuri kwa familia yake na taifa kwa ujumla, kwa sababu yule alikuwa ni KIONGOZI WA KITAIFA.

Lakini hiyo ndio SIASA! Mahasimu wake wa KISIASA ndio waliamua kufanya tukio kama lile, lakini sio vizuri wala sio jambo la kushangilia πŸ™πŸ½

Ile MAKALA YA KISIASA ipo, sema sasa hivi naona SAFARI CHANNEL na TBC1 wameacha kuirusha hewani.
 

Nilivokuwa mdogo nilikuwa nawaza kwanini dingi asijenge nyumba nyinginyingi na maghorofa!!!!, kwanini dingi asinunue magari mengi mengi mengine anigawie !!!!


Nilipokuwa mtu mzima ndo nikajua kumbe dingi hakuwa mzembe...KUTOBOA SIO RAHISI.
 
Ukishakuwa mkubwa utaelewa na inawezekana umenunua kiwanja cha 400 sq metres mwaka huu so unaona kila mtu mzembe..Ukishakiuza ndo utapata majibu huko mbeleni. As umri unavokwenda utaelewa kwanini watu wanaagiza magari halafu wanashindwa kuyatoa bandarini na pesa walishaitenga, utaelewa kwanini unayemzidi pesa leo anaweza kukuzidi pesa mara 100 baada ya miaka kadhaa, na kama Mungu atakujalia kufikia kuwa na busara utaelewa kwamba maisha hayana kanuni. Ila wengi huwa wanakufa bila kufikia stage ya kuelewa yote haya. Na wengine Mungu huwajalia kuyaelewa haya mapema maishani. Tunajifunza kutokana na uzoefu,na uzoefu huja na umri
 
Una masiakhara ubungo kiwanja jero! Hata mabwepande usingepata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…