Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Mwaka 2000 baba yangu alinununua heka 1 kwa laki 5, kule Kimara Suka. Juzi juzi tu kakata kipande kamuuzia tajiri aunganishe na kiwanja alichonunua kala milioni 10. Tena amefanya Siri hakuniambia maana Mimi sikai nae angekuwa mjanja kipindi kile Sasa hivi angekuwa na hela nyingi sana.
nahisi kapunjwa mkwanja
 
Habari wakuu

Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.

Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.

Nimesikitika sanaa.

Uzi tayari ...!
Maisha ni chaguo lako.

Mimi nina babu yangu ( late ) alikuwa Askari Magereza Ukonga, alinunua eneo kubwa tu kama nusu eka Mombasa Ukonga na ndio amejenga hapo.

Ila nina Anko zangu kama wawili.

Hawa MaAnko zangu, Babu wa Magereza ndio aliwasaidia kupata kazi huko huko Magereza.

Wa kwanza yeye alinunua kiwanja Ukonga huko Moshi Bar kitambo sana, wakati bado yuko Magereza akawa akipewa wafungwa wakafanye kazi za jela, anawafanyisha fasta, halafu anawapeleka kwenye kiwanja chake wanajenga.

Siku moja moja kama kawaida, amewapeleka wameloweka zege na kama kaqa, zege halilali. Mpaka usiku hajarudisha wafungwa kambini. Alivyogundulika alifukuzwa kazi ila ana sehemu ya kuishi.

Mwingine yeye kazi huwa anasema aliacha mwenyewe. Tangu miaka ya 90 yuko Dar amepanga tu, dereva daladala lakini hana hata gari la kazi la maana. Anadandia tu.

Hivi karibuni ndio mwanaye mmoja wa kike alipelekwa huko Oman kufanya kazi za ndani, akawa amenunua kiwanja Chanika na kujenga nyumba.

Basi Anko huyo ndio anakaa huko, ukimkuta kijiweni anawatambia madereva wenzio kwamba ,wajiongeze siyo kukomaa tu kwenye magari kizembe, yeye amejenga🤣🤣

Hayo ndio maisha ya waswahili.
 
Dsm Ina mambo ya ajabu sana.

Mtu mmj anachezea vyombo vya Sheria, anatusumbua. Waheshimiwa mahakimu na wanasheria mm napenda kuwaita wasomi....

Kesi ya mtu anasumbua watu 100.. Eti eneo lake... Kiuhalisia vifungu vya Sheria ndiyo vina chelewesha mambo.. nashukuru Sana maguful.. mtu hawez sumbua watu 20 yrs?
 
Habari wakuu

Hapa nilikuwa naweka ligi ya mabishano, hivi inawezekana kweli watu walioingia mjini hapa 1992 mpaka leo 2021 Hana hata kiwanja cha kuzugia kweli, enzi hizo maeneo ya Tegeta, Goba, Kawe, Bunju ilikuwa mapori matupu unafika unafyeka nyasi na kujipa eneo mwenyewe.

Mbaya zaidi ulikuwa ukitaka hata kiwanja cha jero pale Ubungo unapata, Sasa mtu ananiambia kaja DSM 1992 lakini tunaganga njaa hapa, imenibidi nitafakari kidogo.

Nimesikitika sanaa.

Uzi tayari ...!
Ununuzi wa viwanja unahitaji akili ya kuona mbele kwa uchache miaka 10 hadi 15.
Kuna sehemu kunauzwa mashamba leo lakini baadaye kutakuja kupimwa viwanja.
Kunako pimwa viwanja yalikuwa mashamba miaka kadhaa iliyopita.
 
Karibu sana. Aisee utajiri wa kwanza ni kumiliki ardhi. Ardhi kila siku inaongezeka thamani hasa kwa Dar na maeneo jirani.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2]
 
Kuna WATU wameishi KOTAZI mpaka wamestaafu na sasa hivi wamerudi kwao na familia zao! Na wanaanza kutafuta AJIRA tena, kama hawakuwahi kuajiriwa. Yaani fulu komedi [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2][emoji2]
 
Basi. Utakuta mtoa mada ana kiwanja mbondole au mvuti cha hatua 20 kwa 25 anajiona kafiiiiiiiiiiika
 
Back
Top Bottom