Haya ni mazindiko ya kiafrika, roho haikai kwenye mti ila anafanya zindiko anaungana na ule mti ukitaka kumuua ni mpaka ule mti ufe kwanza. Hizi zilitumika kama kinga enzi zile watu wanatekwa maporini safari za miguu hamna magari. Zipo nyingi ambazo nimewahi kuziona in action ni kama;
1. Dawa ya mbio- hii kulikuwa na jambazi sugu wanamtafuta kila wakija akitoka mbio hata mbwa hawafati hiyo speed ya jamaa.
2. Kukosekana kwenye hatari- hii mtu akija akudhuru anakuwa hakuoni, walihangaika na huyo mtu mpaka wakaamua kuua mwanae kwa hasira baada ya kumkosa muhusika kila wakati.
3. Dawa ya kurusha ngumi- hii ukimpiga mtu ngumi anazikwa, inafanya kazi pale tu unapokuwa unaonewa lakini ukianzisha ukorofi utapigwa kama ngoma.
4. Dawa ya kurusha jiwe au fimbo - hii kama mtu kakukimbia na huwezi mpata basi ukichukua kitu chochote ukarushia uelekeo wake humkosi, hata awe mbali wa viwanja 3 vya mpira.
Na zingine kibao kwa nyie watoto wa miaka ya 90 na 2000 hamuwezi elewa.