Biblia sio zao la Rumi na kamwe haitakaa iwe hivyo.Rumi [upapa]hauipendi Biblia kabisa kwasababu inawakosoa na kuwahukumu kwa mengi.Kwa miaka mingi walijaribu kuificha Biblia na na kudhibiti watu wasiwe nayo,lakini MUNGU aliwaibua akina Martin Luther na wengine waliofichua aibu ya Rumi na hatimaye Biblia ilitolewa mafichoni na tunayo hata leo,ingawa bado wanaendeleza mapambano ya kuidhoofisha kwa kuondoa baadhi ya vifungu vinavyo wahukumu [hawata fanikiwa kamwe].
Hicho unachoamini kuwa ni uhalisia [mila,jadi, umizimu n.k.]ni hila za Shetani/Ibilisi ili aendelee kuabudiwa, ana uwezo wa kufanya chochote ili kukuaminisha kuwa unachokiamini ndio uhalisia ilimradi usitoke kwenye himaya/milki yake.
Nyumbani kwa mizimu ni kuzimu yaliko makazi ya Shetani na wafuasi wake na sio Afrika,ingawa aliwahi kuifanya Misri kuwa falme yake [kipindi cha utawala wa Farao],alihamia mataifa mengine [Babeli n.k.]na sasa yupo Vatican.
Biblia sio ya wazungu na wala sio ya warumi,Ni NENO LA MUNGU kwa mataifa yote.