Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Una maana gani haziko wazi?

Kwamba kulitakiwa kuwe na shule kama Jangwani secondary school? Kwamba kuwe na kipindi shuleni na mwalimu anaefundisha “jinsi ya kuweka roho kwenye mti? Una maana hii?

Nimekuuliza kabla, unaelewa nini ukisikia neno Mila? Desturi? Tamaduni?

Wewe kwenye family/ukoo wako hakuna Mila? Desturi? Tamaduni?

Unatambua kila elimu/utaalamu unapatikana kwa mujibu wa taratibu?

Sasa wewe umetafuta lini hiyo elimu ya kuweka roho kwenye mti ukaikosa? Ulifuata masharti na kutimiza vigezo?

Wewe hiyo elimu ya chekechea mpaka ulipoishia, ulikutana nayo barabarani ikakuvagaa ama ulifuatishwa/ulifuata utaratibu, masharti na ukatimiza vigezo ndio ukaipata?
GT = Great Thinker like this one [emoji119][emoji1666]
 
Inawezekana , huku Iringa , mtaa niliopo kuna sehemu panaitwa kigamboni kuna mzee mmoja nisingependa mtaja jina ... Yeye pia alikuwa kama huyo mzee wako ...yeye alikaa mbaka sehemu mbali-mbali za mwili wake zikaanza hadi kutoa wadudu kabisaa lakini bado mzee hakati kambaa (hafii )...

Baadae wanandugu wakaenda kwa mtaalamu kuona shida nini kwa mzee wao anapitia yote hayo ???... Ikabidi aende kwa mtaalamu .

Mtaalamu akawaambia ili mzee wao aweze kufa inabidi wampleke kwenye zile nyumba za udongo kama za duara hivi juu zimeezekwa kwa paa la nyasi wamlaze humo .... Afu mmoja wa wanandugu (ambaye alikuwa ameteuliwa na mtaalamu ) apande juu ya paa la nyumba hiyo na maji maalumu kisha achukue tone moja la maji na alenge kwenye kinywa cha mzee huyo akipatia tu basi mzee ataka moto ,,, unaambiwa hiyo shughuli ya kulenga haikuwa rahisi ... Kwani huyo jamaa ilimchukua siku tatu ndiyo kufanikisha zoezi baada ya hapo ndiyo mzee kufariki....

Hivyo kutokana na story hii hichi ulichokiandik a naweza kuamini kuwa inawezekana.....
 
Usihangaike ,tumwahi Tundu LISu aseme kwasababu haiwezekani yaliyomtokea awe hai mpaka Leo ,Ile haikua ajali ya basi

Kuhusu roho za watu kuwekwa kwenye wanyama au nyikani ipo rejea kipagate mwizi maarufu na serikali hadi wamlimtafutia asali mtingini na akaishi nae miaka zaidi ya 7 ,ndipo ilipogundulika roho yake ipo kivuli Cha kisigino ndipo siku ya harusi polisi wakapiga kivuli Cha kisigino na kufariki yanashangaza ila yapo tunaishi nayo ,hutaki njoo ulishwe ubongo wa fisi hutajutia
"kina kirefu" pekee ni tafsiri ya jinsi ulivyo [emoji1745]

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
 
Hii inanikumbusha mshairi Amir S Andanenga aliwahi kuandika shairi linalohusu haya mambo. Kifupi hawa watu wanaokula dawa wapo.
 
Soma Biblia uielewe ndugu.Imani ya umizimu,ibada ya wafu n.k.ni desturi za kipagani za kirumi [rumi ya kipagani]zilizoingizwa kwy dini [ukristo]kipindi cha utawala wa mwanzo wa upapa sambamba na mengine kadhaa na kufanywa kuwa sehemu ya ibada .
Ni nani mwandishi wa hiyo Biblia?

Rumi hiyo unayosema ya wapagani ndio hii hii inayomiliki Nchi ndani ya Nchi?

Hii hii ambayo inaendesha Siasa za Dunia ya tatu, both Indirectly & Directly?
 
Hayo ni mambo ya kale, maarifa wazee wetu walikuwa nayo miaka hiyo. Sasa hivi vijana hawajui hayo mambo na wanaona ni kama uchawi. 😂😂😂😂

Hata vita vya maji maji, wajerumani walishindwa sema kuficha aibu wakasema wao ndiyo walishinda, ila kiundani sisi tulishinda na ile dawa ya kugeuza risasi kuwa maji ilifanya kazi kweli.
Acha uongo
 
Hiyo ipo hasa kwa watu wenye umri mkubwa ni mambo ya dawa za asili mara nyingi anachukuliwa mgonjwa husika anawekwa ndani alafu sehem ya paa inatobolewa kidogo anapigwa na ule mwaga wa jua akiwa ndani hapo ndio anakata roho vingnevyo ataoza na harufu juu
Na Hilo paa lazima Liwe la nyasi...hizo ni dawa za kujiongezea umri mrefu
 
Hakuna ajabu yoyote ila ni elimu, hio haina tofauti na uhai uliofichwa kwenye sindano na vidonge kwani usipochomwa au kumeza unakufa na ukitumia unapona.
Hivyo kuna tofauti gani na aliyelinda uhai wake kutumia mti?

Nikupe mfano mwingine,
Huyo mzee hata ingetokea ajali asingekufa kirahisi, Je ipi teknolojia bora kati ya hiyo ya kujikikinga na miti au vitu na teknolojia ya Airbag ambayo inapunguza risk wakati wa ajali?
Na hizo dawa ndio zilivo Yani kifo kinakuogopa..Yani kifo hakiji kwa kushtukiza ama kuotewa....
 
Huo uchawi wa kuoza polepole hadi kufa upo na mzee mwenyewe anahusika. Kuweni makini kuna mtu kati yenu anapaswa kurithi huo ushenzi. Wewe kama unanielewa usikubali kamwe kushiriki hizo mila au matambiko mizimu itakuandama. Lakini hata hivyo ukoo wenu ni wachawi sana.
Hiyo hairithiwi kamanda..akifa anaenda zake ...hiyo ni kinga...kinga kwa ajili ya kuongeza urefu wa maisha
 
Hii si vampire/zombie?

Maana katika movies tunaona ndio waathirika wa mwanga wa jua.

Dunia!
Yah ndo izo Hollywood vitu wanatumia sana simulizi za kweli za Africa kutengeneza movies zao mfano black panther,the woman king nk na watu wenye power za ajabu za asili Africa waliokuwepo kibao zamani na Hadi Sasa japo waafrica tumeadaiwa na wazungu na kusahau vitu vyetu Hadi asili yetu,
 
Ni nani mwandishi wa hiyo Biblia?

Rumi hiyo unayosema ya wapagani ndio hii hii inayomiliki Nchi ndani ya Nchi?

Hii hii ambayo inaendesha Siasa za Dunia ya
tatu, both Indirectly & Directly?
Biblia imeandikwa na watu wengi/tofauti na kwa nyakati tofauti pia,miongoni mwao ni manabii na mitume..Pia namaanisha Rumi hii hii ya Vatican/upapa,[kilipo kiti cha enzi cha Shetani]iliyotesa na kuuwa watu wa MUNGU,inayofadhili machafuko [vita,ugaidi,magonjwa, umasikini n.k.] na kujifanya inaombea amani duniani.
 
Haya mambo yapo uchawi tupu, hata ukiona kiongozi kila saa yeye anataka kuombewa tu, mara maaskofu wamshike kichwa aombewe, mara aalike wachungaji wanamuombea yeye tu, jua huyo ni pepo au anatumia nguvu za giza ila hapo anahadaa wananchi tu kujifanya mtu wa Mungu sana kumbe ni wa shetani mwekundu nduuuu, nyokoooo huyo..!!
 
Back
Top Bottom