Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Naona hapa Kuna mtu/kiongozi anatafutwa Ili kutupiwa lawama (Nyerere). Je, DR Congo nao pia ni misingi mibovu Yao iliyowekwa toka uhuru?
Je, hiyo misingi mibovu haiwezi kurekebishwa?

Note: Nakubaliana na wanasema "akili" ndiyo msingi wa Kila kitu.

 
Ni kanuni ya maisha anaetoa ndie anaebarikiwa.
Wazungu uwasaidia waafrika ili wazidi kuwa masikini zaidi,wanajua pesa zinadakwa juu kwa juu then zitarudi Tena kufichwa bank za ulaya na majizi ya Africa
Mbona na sisi tumetoa hapo Uturuki?
 
“Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi”
 
Aisee mkuuu una uchungu sana, mwenyewe ninaumia mno kuona ushenzi unaoendelea miongoni mwetu waafrica,

Nasemaje kwa yeyote atakayepata fursa ya kutimukia nje ya bara hili la shida hasa nch yetu hii asichezee hyo fursa.
Kila leo nawambia wanangu kuwa tafuteni fursa za kwenda Ulaya na marekeani lakini hasa Ulaya ya scandinavian countries
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Umenikumbusha!

Walianza kumtukana eti anataka tunyimwe misaada.
 
Huyo Magufuli nae ni mwehu mwingine wala sio wa kumention humu.Bora hata ungemtaja JK NYERERE ila huyo mwehu anatawala badala ya kuongoza ni kielelezo cha mfalme juha ambae alishawahi pita hapa nchini.
Kwa namna ambavyo Magufuli alikuwa anaipeleka nchi, yaani ndiyo tungezidi kuwa duni zaidi, kwa sababu alikuwa anatumia sana nguvu zaidi kuliko akili.

Wazungu wamefika mahali walipo kwa sababu ya akili, siyo nguvu.
 
Wananchi hawawajibishi viongozi wanategemea miujiza na kudra za Mungu 😀!
.... "Basi tunawaomba waheshimu katiba tu" ....
 
Naona hapa Kuna mtu/kiongozi anatafutwa Ili kutupiwa lawama (Nyerere). Je, DR Congo nao pia ni misingi mibovu Yao iliyowekwa toka uhuru?
Je, hiyo misingi mibovu haiwezi kurekebishwa?

Note: Nakubaliana na wanasema "akili" ndiyo msingi wa Kila kitu.
Kwa Tanzania Mzee Ruksa akaanza kuibomia misingi mibovu,mkapa akaendelea kuisambaratisha, Kikwete akaanza kuijenga upya, Magufuli akajitahidi kuirudisha baadhi ya misingi mibovu ya Nyerere na kuibomia misingi mizuri iliyosnza kujengwa na Kikwete, Mwenyezi Mungu akamstopisha.

Kwabuwezo wa Mwenyezi Mungu katuwekea Mama Samia kurekebisha palipoanza kubomolewa na bwana yule na kuendeleza kuijenga misingi thabiti iiyoanza kujengwa na Kikwete.

Heko mama Samia.
 
Nakataa!

Je, Kenya kuna Nyerere
Congo je
Uganda
Zimbabwe?

Wanachi ndio tatizo! Hatuna akili.
 
Nakataa!

Je, Kenya kuna Nyerere
Congo je
Uganda
Zimbabwe?

Wanachi ndio tatizo! Hatuna akili.
Basi tuseme nchi za Afrika matatizo yetu ni yale yale.


South Afrika iliendelea sana kabla ya Weusi kupewa uongozi
 
Viongozi huwekwa na watu na watu wenyewe ndio sisi so why tusiwabadilishe?
Utawabadilisha vipi wakati wananchi wenyewe waliostahili kuwabadilisha viongozi, hawajitambui na wala hawajui wanatakiwa kuwa na viongozi wa namna gani?

Wananchi wanaosubiria teuzi bila ya kujali anateuliwa na nani, anaenda kufanya nini, au wale wanaosubiria rushwa za wakati wa uchaguzi ili wapate t-shirt au kiongozi wa CCM anayesubiria rushwa toka kwa wagombea ili apate pesa ya kununulia bati za kuezekea kibanda chake, huyo unategemea atakuwa na wazo lolote la kubadilisha viongozi ili kuwapata viongozi wazuri zaidi? Huyu kwake, kiongozi mzuri zaidi ni yule anayempa hongo kubwa zaidi.
 
Msilinganishe mataifa ya Ulaya na Nchi za Africa...

Mataifa ya Ulaya yapo miaka 1000 kabla ya nchi yoyote ya Africa kuanza kuwa nchi, Denmark ndio nchi ambayo bendera yake haijabadilika zaidi ya miaka 500
Nikisema hoja yako ya kipuuzi, unaweza kusema nimekuonea, labda niseme kuwa huelewi chochote.

Ebu nipime uelewa wako kidogo:

Singapore, Malaysia, Thailand, hizi nchi zina umri gani? Unajua kuwa haya mataifa yote tulikuwa kwenye kiwango sawa cha umaskini 1961? Imekuwaje leo UNDP wanasema pale walipofikia Malaysia, wakabakia hapo hapo, wasuendelee zaidi, sisi kwa speed tunayoenda nayo itatuchukua miaka 250?

Vipi kuhusu mataifa kama Misri na India, yameendelea sana kwa sababu nibya zamani sana?

Fuatilia, kuna scientific study kubwa ilikwishafanyika ili kujua kwa nini baadhi ya mataifa ni maskini sana na mengine ni matajiri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…