Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Comment yako hii kuna ujumbe zaidi ya ulichoandika, ingebeba maana kama ungekuwa neutral
 
Asipoelewa hapa tena ndio basi tena hao ndio drawbacks zenyewe
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Mshahara wa mbunge uwe milioni Moja na watumie public transport!

Mkuu lakini na wewe! Hujui hata posho ya laki tatu kwa siku haitoshi?

Kumbuka malalamiko ya wajumbe wa bunge la katiba, walidai laki tatu ilikuwa haiwatoshi, wakapendekeza iongezwe ifike alau laki tano kwa siku.
 
Mpaka sasa Tanzania inasifika kwa kuzalisha nini?
 
Chukulia mfano tu hata hapa Tz, mpaka leo msukuma/mnyakyusa wa huko ndanindani wala hajui kua hii nchi kuna kabila jingine zaidi yao. Hii inafanya kua na fikra mfu kabisa, huna changamoto yoyote utagunduaje vitu??
Mwaka 2020, nilikuwa sehemu fulani wilayani Misungwi mkoani Mwanza. Nilikutana na vijana watu wazima ambao ingawa kutoka hapo mpaka Mwanza Mjini nauli ilikuwa sh 5,000/=, lakini hawakuwa wameshafika Mwanza Mjini. Hata barabara ya lami hawakuwa wameshaiona.

Maghorofa waliyaonea kwenye video.

Tokea amezaliwa, amesoma hadi kuhitimu la saba, kaona na kuzaa, lakini barabara ya lami alikuwa akiisikia tu au kujiona kwenye video, japo Mwanza Mjini ulikuwa ni umbali wa nauli ya sh 5,000/= tu.
 
Nini chanzo cha huo utofauti?
Siunajua ukweli unauma, ila ngoja niseme, ni elimu yenye manufaa wa wote yaani hakuna ujinga nchi nzima, hata ukitengeneza sera unajiuliza hawa watu watazipokeaje maana uchambuzi wake hata kwenye mswada unakuwa wenye manufaa, mfano Sasa wengi wanaangalia taarifa ya habari kama tamthilia Sasa huko kila taarifa ya habari inahojiwa imeleta tija kweli au ni tamthilia, bunge linafanyiwa tathmini za kisomi kila wizara inaleta hoja zenye tija, na wabunge hivyo hivyo hawawezi kuweka watu juani na kutoa hoja za ndiyo Mzee bila kuulizwa hili litafanyika kweli au niusanii.
 
Ndio tatizo hilo sasa, mtu kama huyo hata lami haijui si ataona ni sawa tu kwa hiyo barabara aliyonayo.

Miaka ikienda wajukuu wakija kuiona lami wataanza kujiona ni hamnazo wakati huko kulikojengwa lami, wao waliona mahala wakaiga. Waliona tatizo la barabara wakatafuta soln
 
Muda mwingine nadhani tupo trapped kwenye vicious cycle. Kwa maana ya kwamba mtu let's say hajaajiriwa halafu anaona walioko kwenye payroll Kwa maana ya waajiriwa iwe wanasiasa au watumishi wa kawaida wanavyotafuna pesa za serikali kifisadi , naye automatically ataamini kwamba kumbe mfumo ndio hivi wa kupiga pesa? Kwa hiyo ikitokea ameingia kwenye mfumo wa ajira tayari akiwa na hiyo mentality hata kama alikuwa ni mzalendo na hard working, mambo yanakuwa ni Yaleyale na tunakuwa stagnant kama nchi.
 
Like the son, like the father.

Kunahitajika mapinduzi ya kifikra ili kutoka kwenye huo mzunguko.
 
Hata sisi Nyerere alitakiwa awaache wakoloni kwa muda hadi tupate elimu ya kujisimamia
 
Hata sisi Nyerere alitakiwa awaache wakoloni kwa muda hadi tupate elimu ya kujisimamia
Wapigania Uhuru walikuwa na maono gani wakati walipokuwa wakiendesha harakati za uhuru? Ni nini walichokitarajia kukipata, ambacho wakoloni walikuwa hawawapatii?
 
Wapigania Uhuru walikuwa na maono gani wakati walipokuwa wakiendesha harakati za uhuru? Ni nini walichokitarajia kukipata, ambacho wakoloni walikuwa hawawapatii?
Wapigania uhuru wengi walijawa na chuki dhidi ya wakoloni, walitaka sana wapate madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…