Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Wapigania uhuru wengi walijawa na chuki dhidi ya wakoloni, walitaka sana wapate madaraka
Kumbe si mimi peke yangu niliye na huo mtazamo.

Nilipokuwa shule ya Msingi, kutokana na tulivyofundishwa, niliamini walikuwa wazalendo sana.

Lakini baada ya kukua, nilibaini baadhi ya waliojulikana kama wapigania uhuru walikuwa wabaya sana kuzidi Wakoloni weupe. Walitawaliwa na ubinafsi uliopitiliza.
 
Hawakuwa wazalendo, wao walikuwa wanataka uongozi tu.
Nyerere bila kukoswa koswa pinduliwa asingetoka.

Alitoka ila bado alikuwa na uwezo wa kuamia ie 1992
 
Kuamua ni kuchagua na kuchagua ni kuamua
 

Attachments

  • images.jpeg
    30.1 KB · Views: 1
Sasa apo kuna mabo mengi sana ambayo yametutofautisha mpaka wao wameweza kuwa developed country, hizi zote zinaweza kuwa na sababu nyingi kama internal forec and external force yaan factors ambazo zimechangia
Kwanini Hizo internal na external forces ziwepo kwenye nchi zote za weupe tu tena walioko kwenye mabara tofauti tofauti ila zisiwepo kweye nchi zote zenye waafrika tena sio wa bara moja tu bali kwenye mabara tofauti tofauti.?

Huoni ajabu?
Hakuna cha forces wala nini shida sisi akili zetu zimemzidi nyani kidogo tu.
 
Tafadhali mkuu, usimfananishe mtu mweusi na nyani, tafadhali!

Ni kweli ujinga bado upo, lakini unaweza kutokomezwa ikiadhimiwa.
 
Lazima kuwe na utofauti ili mambo yaende hatuwez tuka wote sawa maana kama ni hivo tutakuwa hakuna maendeleo

Ndo maana kuna wajinga na walevu, kuna tajira na maskini

So hizo force ziko tu hata nchi zetu hz za africa ziko sema tu viongoz wetu ndio ambao wanatuangusha hawana kile cha kupoteza

Wenzetu wazungu wanajali sana maendeleo ya kila mtu sio selfish kama watu weusi na wako well civilized sisi bado

Waafrica bado hatujawa na akili ya kujiongoza wenyewe japokuwa tuna uhuru ila bado tuko nyuma sana
 
Usije ujatamka hayo mbele ya Trump. Alishawahi kutoa kejeli mbaya sana ya kibaguzi dhidi ya Bara la Afrika.

1. Aliziita nchi za Kiafrika "Shithole countries"

2. Alizitukana nchi za Kiafrika kwa kusema "Afrika inatakiwa itawaliwe tena"
 
Wa kuifuta wapo wapi mzee kama unajengewa matundu ya vyoo kwa msaada huku unagawa ma V8 viongozi na wastaafu
Maeneo mengine hata vyoo "havifahamiki", labda siku hizi.

Nilisikia kulikuwa na shirika lililojitolea kuufadhili mradi wa kuwajengea vyoo familia za kijiji fulani kilichopo karibu na ufukwe.

Waliwajengea vyoo vya "kisasa", vyenye sakafu na kuezekwa kwa bati.

Miaka miwili baadaye waliporejea kutathmini mradi walioufanya, walikuta hali ni kinyume chake. Hakukuweko na vyoo. Matundu yalikuwa yamezibwa na kugeuzwa makazi.

Walengwa wa huo mradi hawakuona sababu za kuwa na vyoo vya kisasa wakati wanaishi kwenye nyumba za nyasi zisizo na sakafu, na huku vyoo vyao vya asili (vichaka na kwenye maji), vingalipo.
 
 
Aisee mkuuu una uchungu sana, mwenyewe ninaumia mno kuona ushenzi unaoendelea miongoni mwetu waafrika,

Nasemaje kwa yeyote atakayepata fursa ya kutimukia nje ya bara hili la shida hasa nch yetu hii asichezee hyo fursa.
Ni mtu kama wewe, mwenye uchungu na nchi yake ndiye anayeweza kuchochea mabadiliko.

Ukiona unaumia kwa yanyoendelea, ni dalili kuwa mabadiliko yanahitajika, na yapo katika uwezo wako.

Ukweli ndiyo huo. Utafanyaje? Utaendelea kukaa kimya huku mambo yakienda kombo?

Mtu mmoja alishawahi kusema, WATU WEMA WAKIKAA KIMYA, WAOVU HUSHAMIRI.

Usiwe idle, FANYA jambo kwa mustakabali wa vizazi vya Sasa na baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…