Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Tatizo letu ni misingi mibovu iliwekwa toka tulipopata uhuru.
Sidhani ni tangu tulipopata uhuru, sema tangu tulipozaliwa.

Maana kama ni misingi mibaya baada ya uhuru, mpaka leo ni miaka mingapi? Hiyo misingi mibaya kwa nini haibadilishwi? Mbona mataifa mengine yaliyopata uhuru baadaye, kama Botswana na Namibia, wao angalao wanapiga hatua kwa kasi?
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
 
Miaka ya nyuma, wakurugenzi wa Halmashauri walikuwa na kawaida ya kukusanya mafungu ya kuwapelekea wabunge ili mambo yawawaendee sawa wakati wa bajeti, hivi huo ujinga ulishaishaisha?
Sisi tunaangushwa na viongozi wetu, kupitishatu bajeti mpaka wabunge wahongwe. Yaani Africa tumelogwa na nani?
 
Mnaonaje katiba ijayo tuwe na kipengele Cha kusajili viongozi, Kama mawaziri, wakuu wa wilaya, Kama ifanywavo kwenye football.

Tuna mchukua mtu kwenye Kariba ya kiduku😀 tunamkabithi wizara kiroho Safi, tuna achana na hawa wanaoiba huku, kesho wahamishiwa Kule wakaibe Tena.

Rais pekee ndio tunampigia kura
 
Denmark wanaweza kugeuza mchanga/udongo kuwa mashine, Tanzania hatuwezi kugeuza mchanga/udongo kuwax mashine.

Sababu ya pili utawala bora.

Tatu wasomi wao hawalink tumbo na akili katika kudadavua hoja huku kwetu tumbo ndio linaaamua upi uwe ukweli na upi usiwe ukweli sio brain.

Mwisho, huku kwetu wizi ndio primary factor katika kuamua kipi kifanyike na kifanyike n.amna gani, wao determinant ni wap kuna manufaa makubwa zaidi kuliko kwingine wanapotaka kuchagua wafanye kipi.
 
Mkuu, vipi ukilinganisha Tanzania na kanchi kadoogo, Rwanda?

Ni ndogo kieneo, na rasilimali zake ni chache mno ukilinganisha na Tanzania, lakini unaionaje?

Imeshapitia misukosuko migumu mno, lakini...

Nakubaliana nawe, utajiri mkubwa ni AKILI!!!
 
Mifumo ya Europe na kwetu ni tofauti kabisa.Uwajibikaji uko juu sana.kwa pande zote kwa serikali na kwa wananchi

Huko Ulaya wanachi wanaogopwa sana na wanasiasa huku kwetu wanasiasa wanaogopwa sana na wananchi.

Yaani Serikali unaiweka madarakani mwenyewe halafu ikishaingia inaanza kukukupa vitisho ukiihoji

Tanzania ni nchi ya matamko,vitisho na upigaji kwa ngazi zote
 
Kuna mwamba alisema Afrika hasa kusini mwa jangwa la sahara tukihamishiwa nchi za Ulaya nao wakaletwa kuishi hapa Afrika... Kwamba baada ya miaka 5 tutakuja kuomba msaada nilicheka sana... Ila ni kama. Kuna ukweli ndani yake

By the way... Kwanini wanafunga ubalozi wao!??
 
Kumbe sote bas hatuna akili[emoji848][emoji848] maana sijui whats wrong with Africa... Au ndivo tulivo na tusijaribu kujilinganisha nao
May be sisi tumeumbwa tuwe nyuma
 
Naunga mkono hoja.
 
Kwa ufupi mtu mweupe kabarikiwa. Na zaidi sisi mijitu mieusi tunateswa na ubinfsi. Angali kiongozi wetu ananunua goli million 20 nchi gani taifa gani raisi ananunua goli la timu ya klabu kama sio ufisadi nini
Just imagine... Unanunua tiketi kwa ajili ya watu ambao wangeweza kujinunulia tiketi... What a wastage of resourses any way yani Muumba aje tu atutwae wote[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Umemaliza kila kitu hapa
Utajiri na rasilimali muhimu ni watu watu wenye akili ya kuchanganua mambo na kutatua changamoto zinazowazunguka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…