Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Siyo Denmark pekee. Vinchi vyote vidogo huko Ulaya, na baadhi huko Asia, ukilinganisha na Tanzania ni aibu tupu:

Denmark
Norway
Finland
Sweden
Singapore
Switzerland

Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.

Hata upewe vyote, ukinyimwa akili, vyote vinakuwa havina maana. Lakini ukibahatika ukapata akili,ni mwanzo wa mafanikio yote. Kwanza utajua ni nini kilicho muhimu, utakuwa na mifumo mizuri ya kuvuna rasilimali, utakuwa na tekinolojia, utakuwa na mifumo mizuri ya utawala, na mifumo mizuri ya kusimamia uchumi kwa ujumla.

Sisi tuna vitu vingi, lakini asilimia kubwa sana ya watu wetu wamenyimwa akili, utashi na maarifa. Ndiyo maana wachache wenye akili, maarifa na utashi, ama wanakuwa frustrated na kukata tamaa au kuishia kwenda kufanya kazi mataifa ya nje kwa sababu nchini mwao ni giza nene.
Wakitokea viongozi wenye akili kubwa hawakawii kuitwa madikteta na hawakawii kuuliwa ili wapumbavu waendelee kushika dola.
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
China ilikua na uchumi uliokaribiana na WA TANGANYIKA 1961,

Back in 1960 — sixty-two years ago — China was poorer than most African countries. Per capita income in China in 1960 was US$89. Congo, Cote d'Ivoire, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Senegal, and South Africa were all richer than China.

That's what happened 😭😭😭
 
China ilikua na uchumi uliokaribiana na WA TANGANYIKA 1961,

Back in 1960 — sixty-two years ago — China was poorer than most African countries. Per capita income in China in 1960 was US$89. Congo, Cote d'Ivoire, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Senegal, and South Africa were all richer than China.

That's what happened 😭😭😭
Kama tumeshindwa kujifunza kwa Mzungu kwa kuwa hatumwamini beberu, basi tukajifunze kwa Mchina "tunayemwamini" kuwa ni rafiki wa kweli!

Hali yoyote ile, utajiri au umaskini, husababishwa, hivyo inawezekana kujifunza pia kufanikiwa au kutofanikiwa.
 
Kama tumeshindwa kujifunza kwa Mzungu kwa kuwa hatumwamini beberu, basi tukajifunze kwa Mchina "tunayemwamini" kuwa ni rafiki wa kweli!

Hali yoyote ile, utajiri au umaskini, husababishwa, hivyo inawezekana kujifunza pia kufanikiwa au kutofanikiwa.
Hata viongozi waheshimiwa wengi wakitaifa wakiulizwa Tatizo ni nini hawana JAWABU 👀👀
 
Kwanini Hizo internal na external forces ziwepo kwenye nchi zote za weupe tu tena walioko kwenye mabara tofauti tofauti ila zisiwepo kweye nchi zote zenye waafrika tena sio wa bara moja tu bali kwenye mabara tofauti tofauti.?

Huoni ajabu?
Hakuna cha forces wala nini shida sisi akili zetu zimemzidi nyani kidogo tu.
Nchi zako Zina umri Gani?
 
Mambo gani yame badilika 🤔
Watu wameshaanza kuamka. Sasa ni tofauti kidogo na zama za ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI. Si unaona hata wewe mwenyewe unavyokwazika?

Mimi naamini, siku za mbeleni, tena siyo mbali saana, hali itakuwa tofauti sana. Fikra mpya na chanya zinaendelea kuibuka.
 
Samahani mkuu, naomba nikuulize kama hutojali. Wewe ni Mzungu au Mweusi?

Ila samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
Najua lengo la swali lako.
Kwamba kwa vile mim ni mweusi nipingane na ukweli kuwa mtu mweusi ni janga na hana akili.

Natamani kupinga na kusema kwa fuahari kuwa mim mtu mweusi ni bora na mwenye akili kama binadamu wengine wote ila nafsi inanisuta sababu sio kweli na hata nikijidanganya kuwa nina akili kama wazungu haitasaidia kitu.
 
Rushwa na uzembe ni miongoni mwa sababu zinazoturudisha nyuma sisi hapa Tanzania.
Sababu nyingine ni ufisadi miongoni mwa watumishi wa serikali.
JamiiForums1309756111.jpg


Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
Labda kama unamaanisha Chato kuwa kama Ulaya
 
Back
Top Bottom