Ni kweli india wana dawa nyingi sana za herbal kwa sababu wamewekeza zaidi kwenye research.Huwezi kufahamu aina nyingi na tofauti za mitishamba bila kuwekeza kwenye utafiti vinginevyo utabaki kutapeli watu tu.Hata hapa Tanzania dawa zipo za kila aina isipokuwa pia watanzania wengi hatuaminiani sisi kwa sisi,mtanzania akiwa na shida ya ugonjwa ukamwambia ugonjwa huu utapona kwa dawa hii wasiwasi ni mwingi kuliko akiambiwa na ngozi nyeupe.Hizo dawa mnazowasifia wahindi wakati mwingine ni hizihizi aina ya mitishamba yetu na wako hapa kila siku kuvuna.Dawa za madonda ya tumbo,kisukari,presha n.k ni za kawaida sana na wanazivuna katika mazingira yetu wanaboresha muonekano ndiyo maana wanaaminika.Amini usiamini dawa ni hizi hizi na wanavuna humuhumu kwetu.Mimi nina marafiki zangu wengi wa rangi hiyo tunapambana nao hapahapa na wakati mwingine wanapenda sana kujifunza kupitia kwetu na wanachukua maarifa yetu na kuyawekeza vizuri zaidi.