India na dawa nzuri sana za miti shamba,

Ni kweli india wana dawa nyingi sana za herbal kwa sababu wamewekeza zaidi kwenye research.Huwezi kufahamu aina nyingi na tofauti za mitishamba bila kuwekeza kwenye utafiti vinginevyo utabaki kutapeli watu tu.Hata hapa Tanzania dawa zipo za kila aina isipokuwa pia watanzania wengi hatuaminiani sisi kwa sisi,mtanzania akiwa na shida ya ugonjwa ukamwambia ugonjwa huu utapona kwa dawa hii wasiwasi ni mwingi kuliko akiambiwa na ngozi nyeupe.Hizo dawa mnazowasifia wahindi wakati mwingine ni hizihizi aina ya mitishamba yetu na wako hapa kila siku kuvuna.Dawa za madonda ya tumbo,kisukari,presha n.k ni za kawaida sana na wanazivuna katika mazingira yetu wanaboresha muonekano ndiyo maana wanaaminika.Amini usiamini dawa ni hizi hizi na wanavuna humuhumu kwetu.Mimi nina marafiki zangu wengi wa rangi hiyo tunapambana nao hapahapa na wakati mwingine wanapenda sana kujifunza kupitia kwetu na wanachukua maarifa yetu na kuyawekeza vizuri zaidi.
 
Ni kweli ila kuwa makini na impostors wanaojifanya wanauza dawa za Himalaya
 
Watakuja kufahamu muda umesogea.Hatari sana! Yaani mtu anaiamini herbal kwa sababu ni ya mhindi.
Nisha zitumia sana na nina watu wanazitumia, India inahadi Hospitali za kutibu kwa Madawa ya asili, Uliza Raila Odinga yule Binti wake alienda kuponea Macho India.
 
Ni kweli kabisa, kuna dawa za asili za India nimezitumia mara kadhaa kwakweli ni nzuri sana (asili sio miti)

Kuna kidonge kipo kama chocolate flani hivi nmesahau jina ni cha kikohozi unakiweka tu chini ya ulimi kinayeyuka, perfect inatibu chaaap.
Mafua na vikohozi kwangu ni shida kuliko malaria. Fanya kushare nami hiyo dawa
 
India ndio duka la dawa la dunia. Mataifa mengi sana ikiwemo mataifa makubwa kama Marekani na China wanategemea kwa kiasi fulani, kuingiza dawa kutoka India.​
 
Mafua na vikohozi kwangu ni shida kuliko malaria. Fanya kushare nami hiyo dawa
Yani hata jina siikumbuki ngoja nisake box lake kama nitalipata....ukiiweka chini ya ulimi tu kesho unaamka mpya.
 
Tz kuna dawa nying sana za asili ila hatujafanikiwa kuziprocess na kuzihifadh na kuweka kwenye mfumo mzur kama india na mataifa mengne.

Nyongeza
India wanasumbuliwa sana na magonjwa ya lishe hasa sukari
 
Mkuu nicheki namba yangu hii kuhusu iyo dawa za India ntapataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…