PreGE2025 INEC: Chama kisichosaini kanuni za maadili ya uchaguzi, hakitashiri Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ila ccm wana hila za kijinga sana! Yaani uchaguzi unafanyika mwishoni mwa mwezi wa 10, halafu unaweka sharti la kusaini hizo kanuni mwezi wa 4! Na chama kinachoshindwa kusaini, eti kinanyimwa/kinakosa haki ya kushiriki uchaguzi!!

Hii nchi inahitaji mabadiliko ya kweli. Hali hii ikiendelea kuwa hivi, hatutafika.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima amesema kwa mujibu wa kanuni Chama kisichosaini kanuni za maadili hakitashiriki uchaguzi.

“Chama cha siasa ambacho hakita saini kanuni za maadili ya uchaguzi kesho hakitapata fursa ya kushiriki uchaguzi mkuu…” - Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima akizungumza katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Chama kisichosaini hakitapata fursa ya kusimamisha uchaguzi.

Kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT, inatambua uwepo wa Tume ya Uchaguzi, yaani NEC LAKINI siyo Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). INEC kwa mujibu wa Ibara hiyo ya Katiba ni Kitu BATILI kwani haitambuliki na Katiba. Marekebisho ya jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC yalipaswa kutanguliwa na Marekebisho ya Katiba iliyopo kwanza, hususani Ibara hiyo ya 74.

Katiba inasema kwamba kutakuwa na Tume ya Uchaguzi wala siyo Tume Huru ya Uchaguzi. Mabadiliko haya ya Sheria ya Uchaguzi yaliyosababisha kubadilisha jina la Tume ya Uchaguzi kutoka NEC kwenda INEC ni BATILI kwa mujibu wa Ibara hiyo ya 74 kwani Mabadiliko haya yanakinzana na matakwa ya Katiba ya nchi.

Kwa maana hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) ni Taasisi au kitu ambacho hakitambuliki na Katiba ya nchi hivyo ni BATILI KWA UJUMLA WAKE. Taasisi hiyo haitambuliki kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT
 
Back
Top Bottom