Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mimi maji ninayopendelea kunywa tangu nafika Dar es Salaam ni maji brand ya Uhai, yalipokuja Hill water niliyapenda kwa sababu ya muonekano wa chupa yake na portability yake. Nimeona matangazo ya maji mengi lakini sijawahi kufikria kununua maji kwa sababu ya kushawishiwa na influencer.
Nimekuwa mpenzi wa Pepsi muda mrefu kabla hata Diamond hajaanza kutangaza Pepsi, Nimekuwa nakunywa maziwa ya Tanga Fresh na ASAS kabla ya kumjua hata influencer mmoja anayetangaza haya maziwa. Sijawahi kwenda duka fulani kwa sababu ya kelele za Influencer yeyote.
Hivi kiuhalsia inawezekana kweli mtu anaenda kununua bidhaa fulani kwa sababu ya Mwijaku, Baba Levo, Manara, Diamond n.k Yani mtu anaweza kuhama kutoka NMB kwenda CRDB kwa sababu ya Ali Kamwe bila kulinganisha huduma na kuona ipi inamfaa?