Unaweza usielewe wala kuamini, lakini influencer wana mchango mkubwa sana kuuza bidhaa za makampuni. Ngoja nikupe shule ndogo kidogo;
1. Katika kufanya maamuzi, binadamu huongozwa na kitu kinaitwa Conscious (ufahamu huku ukijua) na Subconscious (ufahamu pasipo kujua), hao influencor kazi yao kubwa ni kuweka hints ya taarifa kwenye ubongo wako, na hiyo hubakia kama rejea (reference) itakayokuathiri wakati wa kuamua kununua kitu. wasipo kupata katika conscious basi wanaweza kukupata kupitia Subconscious. Hata kama hutanunua bidhaa wanayoitangaza (kwa sababu fulani mahususi uliyokwisha kuijenga) utajikuta wewe mwenyewe unanunua bidhaa nyingine lakini huku ukijua kabisa unaikwepa kimakusudi ile bidhaa iliyokuwa inatangazwa na influencer!
2. Katika sayansi ya biashara, huenda 90% ya wanunuzi huwa ni 'wajinga' wakati wa kununua, hununua bidhaa kwa kuaminishwa ni nzuri, bora au nafuu. Na imani hiyo huletwa kwa kusikia au kwa kuona watu wanaowaona au kuwasikiliza mara kwa mara. Mtu mwenye followers zaidi ya laki moja mtandaoni, maana yake ana watu laki moja wanaoweza kusilikiza chochote anachokileta, kuiga, kumuunga mkono nk. Ukikaa wewe mwenyewe binafsi halafu tafakari, utagundua kuna wakati maishani mwako uliwahi kununua kitu fulani kwa 'ujinga' tu, yaani kwa kuiga tu mtu au watu fulani, kuambiwa tu ni kizuri, bora au nafuu bila ya wewe mwenyewe kuchunguza kwa kina.