Infosys IPS (T) LTD wakanusha kuhusika na LUGUMI katika kashfa ya ubadhirifu

Infosys IPS (T) LTD wakanusha kuhusika na LUGUMI katika kashfa ya ubadhirifu

Kitwanga ndio anajaribu kujisafisha. Haya bana hata Yusuph manji hausiki kabisa na quality group kwa sasa. Hiyo infosy ni Mali ya kitwa ga
Umeshaambiwa Kitwanga ni founder, ila kwa sasa sio Director, hivyo kibiashara anasubili gawio la faida mwisho wa mwaka.

Ok, hata kama Kitwanga angekuwa ni Director kwa sasa, bado wameweka mambo wazi kama infosys, ambayo yako crystal clear.

Watanzania wengi tunapelekwa na matakwa ya wanasiasa, Lowasa alivyokuwa CCM tuliambiwa ni fisadi, tukimuona tumzomee, ameingia CHADEMA amekuwa msafi kama malaika.

Vijana tuache kutumika katika siasa!
 
2010 mkuu kamwaga manyanga Infosys.... 2011mkwe wa IGP mtoto wa mfalme lugumi kapewa tenda na jeshi la polisi...biometrica wanawafuata Infosys kupitia website yao na kuwapa deal....Ok..
 
Huyu naibu meneja mwenyewe amekaa kidalaridalari.
 
Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.

Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
nlijua tu wanataka kukifanya kile walicho fanya kipindi kileee cha kashifa ya ESCROW, hasa kwa wivu, na wakawatumia wabunge kuiyumbisha serikal, bt nw hawawezi, wameshindwa kwa wabunge maana hata wa upinzani sasa hivi wanaona aibu wataanza vipi? ila ukwel ndo huo umesemwa watafute lugha nyingine
 
Kampuni ya INFOSYS IPS (T) LTD imekanusha taarifa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwamba kampuni hiyo inahusika na inashirikirikiana na Lugumi Enterprises katika kashfa ya ubadhirifu.

Katika habari zilizosambaaa inasemekana kwamba kampuni ya Infosys ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka katika kampuni ya Lugumi, jambo ambalo wao wanadai si la kweli na ni la kupuuzwa na umma.

'Hatujawahi kufanya biashara na kampuni ya Lugumi Enterprises' Amesisitiza Bwana Sweki Donald, Naibu Meneja Mkuu Infosys IPS (T) LTD.

Video:

Katika hali ya kawaida tu wewe ulitegemea wangekubali kuwa walihusika kwenye Mkataba wa Lugumi ???????
 
a)Lugumi kakimbia nchi
b)Mkataba ukaenda kamati nyingine ambayo haikuuomba
c)Halafu kanusho la uhusika ndio linatoka
ahahaha
nimempenda director wa hii movie
 
Kampuni ya INFOSYS IPS (T) LTD imekanusha taarifa zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kwamba kampuni hiyo inahusika na inashirikirikiana na Lugumi Enterprises katika kashfa ya ubadhirifu.

Katika habari zilizosambaaa inasemekana kwamba kampuni ya Infosys ilipokea mabilioni ya shilingi kutoka katika kampuni ya Lugumi, jambo ambalo wao wanadai si la kweli na ni la kupuuzwa na umma.

'Hatujawahi kufanya biashara na kampuni ya Lugumi Enterprises' Amesisitiza Bwana Sweki Donald, Naibu Meneja Mkuu Infosys IPS (T) LTD.

Video:

Mkuu Infomer asante kwa hii.

Naomba nisaidie hapa,

Mwenye deal ya supply ni Lugumi, supplier ya Biometrica ya US, Lugumi amekwenda ili auziwe, lakini Lugumi hawezi kufanya physibility study ya needs and assesment, ndipo huyo Biometrica akawatafuta Infosis na kuwapa kazi ya kufanya study ya Needs and Assesment kwenye vituo vya polisi 108. Alipokamilisha kazi yake, akalipwa!.

Hili la Kitwanga kuwa ni mmiliki halina tatizo as long as baada ya kuingia kwenye siasa, aliacha kushughulika na kampuni.

Kikweli nimemuona huyo meneja anajiuma tuu kuhusu Kitwangwa na alipoulizwa kama Kitwanga anafika hapo, alidanya wazi kuwa hajawahi kufika tena kitu ambacho hakiwezi kuwa kweli!. Kutokujishugulisha na biashara is one thing na kufika hapo is another.

Kwenye issues kama hizi wahusika hushauriwa kuwa very brief, ukiishasema infosis haikupewakazi na Lugumi bali imepewa na Biometrica, ilitosha, huyo meneja hakupaswa kuongeza neno baada ya hapo, anawezakujikuta anajikanyaga mwisho akaharibu.

Pasco
 
Umeshaambiwa Kitwanga ni founder, ila kwa sasa sio Director, hivyo kibiashara anasubili gawio la faida mwisho wa mwaka.

Ok, hata kama Kitwanga angekuwa ni Director kwa sasa, bado wameweka mambo wazi kama infosys, ambayo yako crystal clear.

Watanzania wengi tunapelekwa na matakwa ya wanasiasa, Lowasa alivyokuwa CCM tuliambiwa ni fisadi, tukimuona tumzomee, ameingia CHADEMA amekuwa msafi kama malaika.

Vijana tuache kutumika katika siasa!
Kitwa -ga anahusika sana na hiyo infosy,na alihusika kutengeneza hill deal
Nadhani weweni moja wapo mnaotumiwa na mawe matatu mumtete huku kwenye mitandao.
Kwa taariga yako huyo muheshimiwa yupopia kwenye list ya watumishi hewa wa bot.
Acha kutumika vibaya.
 
Haya sasa ukweli umewekwa wazi kumbe ni juhudi za kumpiga vita Waziri Kitwanga na kutaka kuichafua serikali ya Magufuli.

Wapiga dili tafuteni kiki nyingine ukweli ndio huu.
Toka lini kukanusha kukawa ndio ukweli? Hata Babu Seya alikanusha kubaka na bado akafungwa........BTW huyo msemaji mbon hasemi uhusikaji wa Kitwanga na kampuninya Infosys?
 
Huu Uzi umeanzishwa na kitwanga ili ahadae watanzania.chief!hana pakutokea kwenye hili sakata la lugumi!

Comrade, nadhani huna uhakika na unachosema.
 
Mkuu wakati Magufuli na serikali yake wakipambana kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa juhudi kubwa kuna watu wanapambana kuona hafanikishi hilo kwa manufaa ya vyama vyao na dili zao. Kelele nyingi ila ndio mafisadi wakubwa tungewaachia funguo ya hazina tungejuta sisi na vizazi vyote.
Acheni kutafuta mchawi,acheni kuwasingizia wapinzani,acheni kutafuta huruma kwa wananchi, acheni kutuona wajinga.

You can fool some people some times,but You cant fool all the people all the time!
 
Mbona kama ESCROW vile na ile ngonjera yao ya fedha ni ya umma, sio fedha ya umma
 
1. Wewe ni waziri tena wa wizara ambayo kampuni uliyoianzisha wewe wana mahusiano ya kibiashara. Je huoni kwamba kuna mgongano wa kimaslahi?

2. Ikiwa wizara yako imetangaza tenda kampuni yangu ikatenda na Infosys uliyoianzisha wewe ikatenda, naweza kupewa mimi? Hata nikikosa kwa haki na ikapata Infosys nitaridhika?

3. Hivi ni sahihi kampuni zenye mahusiano na mawaziri kufanya kazi na serikali wanayoitumikia?

4. Kampuni yako imekanusha kuijua wala kushirikiana na Lugumi. Wewe binafsi unaijua Lugumi na wamiliki wake? Kama unaijua inawezekanaje watu wa kampuni uliyoianzisha hawaijui?

5. Kelele kubwa zinaendelea kuhusu wizara unayoiongoza, kimya chako kinasababishwa na nini? Mbona hujatoka hadharani kuzungumza lolote kuhusu kinachoendelae ofisini mwako?

6. Unasubiri kutimuliwa? kwa nini usimwombe bwana mkubwa akuweke pembeni ili uchunguzi uendelee vizuri ofisini kwako?

7. Ni kweli kwamba una uhusiano/rafiki wa karibu na bwana mkubwa?

8. Uhusiano huo kama upo ni wa kawaida au wa kibiashara?

9. Kama ni wa kibisahara anahusika kwenye Infosys?

10. Kama mna uhusiano kama inavyosemekana huoni kwamba unampa mtihani mkubwa sana rafiki yako?
 
Umesahau swali mmoja: je una uhusiano wowote wa kibiashara na mzee wa Msoga?
 
Back
Top Bottom